Kumbukumbu la Torati 10
10
Jozi ya pili ya mbao
1 #
Kut 34:1,2; 25:10 Wakati ule BWANA akaniambia, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, kisha uje kwangu huku mlimani, ukajifanyie na sanduku la mti. 2Nami nitaandika juu ya hizo mbao maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, ulizozivunja, nawe uzitie ndani ya hilo sanduku. 3#Kut 25:5; 37:1 Basi nikafanya sanduku la mti wa mshita, nikachonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, nikakwea mle mlimani, na zile mbao mbili mkononi mwangu. 4#Kut 34:28; Yer 31:33; Kut 20:1; 19:17; Kum 9:10; 18:16 Naye akaandika juu ya mbao mfano wa maandiko ya kwanza, zile amri kumi,#10:4 au maneno kumi. alizowaambia BWANA huko mlimani kutoka kati ya moto siku ya mkutano; BWANA akanipa. 5#Kut 34:29; 40:20; 1 Fal 8:9 Basi nikageuka nikashuka kutoka mlimani, nikazitia mbao ndani ya sanduku nililofanya; nazo zimo humo kama alivyoniamuru BWANA. 6#Hes 20:28; 33:31,38 (Wana wa Israeli wakasafiri kutoka visima vya Bene-yaakani kwenda Mosera; Haruni akafa huko, akazikwa huko; na Eleazari mwanawe akahudumu kama kuhani badala yake. 7Wakasafiri kutoka huko kwenda Gudgoda; wakatoka Gudgoda wakaenda Yotbatha, nayo ni nchi ya vijito vya maji. 8#Hes 3:5-8; Law 9:22; Hes 6:23; Kum 21:5 Na wakati huo BWANA alilitenga kabila la Lawi ili walichukue lile sanduku la Agano la BWANA, wasimame mbele ya BWANA kwa kumtumikia, na kuwabarikia watu kwa jina lake, hata hivi leo. 9#Hes 18:20,24; Kum 18:1,2; Eze 44:28 Ndipo asiwe na fungu Lawi, wala urithi pamoja na nduguze; BWANA ndiye urithi wake, kwa mfano wa vile alivyomwambia BWANA, Mungu wako.) 10#Kut 34:28 Nikakaa mle mlimani kama hapo kwanza, siku arubaini usiku na mchana; BWANA akanisikiza wakati huo nao; BWANA asitake kukuangamiza. 11BWANA akaniambia, Ondoka, uendelee na safari yako ukiwaongoza watu; nao wataingia waimiliki nchi, niliyowaapia baba zao ya kuwa nitawapa.
Umuhimu wa kuwa na amri
12 #
Mik 6:8; Yer 7:23; Mt 22:37; 1 Tim 1:5 Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; 13kuzifuata amri za BWANA na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri? 14#1 Fal 8:27; Zab 115:16; Mwa 14:19; Zab 24:1 Tazama, mbingu ni mali ya BWANA, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo. 15Tena, BWANA aliwafurahia baba zako, na kuwapenda, akawachagua wazao wao baada yao, naam, na ninyi zaidi ya mataifa yote kama hivi leo. 16#Law 26:41; Yer 4:4; Rum 2:28; Efe 4:21; Kol 2:11 Basi, zitahirini govi za mioyo yenu, wala msiwe na shingo ngumu. 17#1 Tim 6:15; Ufu 17:14; 19:16; Mdo 10:34; Rum 2:11; Zab 136:2; Dan 2:47; 2 Nya 19:7; Ayu 34:19; Gal 2:6; Efe 6:9; Kol 3:25; 1 Pet 1:17 Kwa maana BWANA, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea watu, wala kukubali rushwa. 18#Zab 68:5; 146:9 Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. 19Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri. 20#Mt 4:10; Zab 63:11 Mche BWANA, Mungu wako, umtumikie yeye; ambatana naye, na kuapa kwa jina lake. 21#Zab 22:3; Yer 17:14 Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako.
22 #
Mwa 15:5; 22:17; 46:27 Baba zako walienda Misri wakiwa watu sabini; na sasa BWANA, Mungu wako, amekufanya kama nyota za mbinguni kwa wingi.
Iliyochaguliwa sasa
Kumbukumbu la Torati 10: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.