Kumbukumbu la Torati 26
26
Mavuno ya kwanza na fungu la kumi
1Na itakuwa, ukiisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi, na kuimiliki, na kukaa ndani yake; 2#Kut 23:19; Hes 18:13; Mit 3:9; Rum 8:23; 1 Kor 15:20; Yak 1:18; Kum 12:5 twaa malimbuko ya ardhi, utakayoyavuna katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako; ukayatie katika kikapu, ukaende hata mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wako, ili alikalishe jina lake huko. 3Ukamwendee kuhani atakayekuwapo siku zile, ukamwambie, Ninakiri leo kwa BWANA, Mungu wako, ya kuwa nimeingia katika nchi BWANA aliyowaapia baba zetu ya kwamba atatupa. 4Naye kuhani atakipokea kikapu mkononi mwako, akiweke chini mbele ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako. 5#Mwa 26:5; 28:5; Hos 12:12; Mwa 43:1,2; 45:7,11; 46:27; Kum 10:22 Nawe ujibu, ukaseme mbele za BWANA, Mungu wako, Baba yangu alikuwa Mwarami karibu na kupotea, akashuka Misri, akakaa huko ugenini, nao ni wachache hesabu yao; akawa taifa kubwa huko, yenye nguvu na watu wengi. 6#Kut 1:11 Wamisri wakatuonea, wakatutesa, wakatutumikisha utumwa mzito. 7#Kut 2:23-25; 3:9 Tukamlilia BWANA, Mungu wa baba zetu; BWANA akasikia sauti yetu, akaona na taabu yetu, na kazi yetu, na kuonewa kwetu. 8#Kum 4:34; 34:11,12 BWANA akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa utisho mwingi, na kwa ishara, na kwa maajabu; 9#Kut 3:8 naye ametuingiza mahali hapa, na kutupa nchi hii, nchi ijaayo maziwa na asali. 10#Kum 8:18; Mit 10:22 Na sasa, tazama, nimeleta malimbuko ya mazao ya ardhi uliyonipa, Ee BWANA. Kisha ukiweke chini mbele za BWANA, Mungu wako, ukasujudu mbele za BWANA, Mungu wako; 11#Kum 12:7,12,18; Mhu 5:18-20; Isa 65:14; Mdo 2:46,47; Flp 4:4; 1 Tim 6:17; Zab 63:3,5 ukayafurahie mema yote ambayo BWANA, Mungu wako, amekupa, na nyumba yako, wewe, na Mlawi, na mgeni aliye kati yako.
12 #
Kum 14:28-29; Law 27:30; Hes 18:24 Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za mavuno yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba; 13#Zab 119:141,153,176 nawe sema mbele ya BWANA, Mungu wako, Vitu vilivyo vitakatifu nimeviondoa katika nyumba yangu, nami mimewapa Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, kwa mfano wa maagizo yako uliyoniusia yote; sikukosa maagizo yako yoyote, wala sikuyasahau; 14#Law 7:20; 21:1,11; Hos 9:4 katika vitu hivyo sikula wakati wa kukaa matanga mimi, wala sikuviondoa nikiwa na unajisi, wala sikutoa kwa ajili ya wafu katika vitu hivyo; sauti ya BWANA, Mungu wangu, nimeisikiza, nimefanya yote, kama ulivyoniamuru. 15#2 Nya 6:26,27; Zab 80:14; Isa 1:2; 57:15; Zek 2:13; Mdo 7:49 Uangalie kutoka makazi yako matakatifu mbinguni, uwabarikie watu wako Israeli, na nchi uliyotupa kama ulivyowaapia baba zetu, nchi imiminikayo maziwa na asali.
Mausia ya mwisho
16Leo hivi akuamuru BWANA, Mungu wako, kuzifanya amri hizi na hukumu; basi uzishike na kuzifanya kwa moyo wako wote na roho yako yote. 17#Kut 20:19; Zab 48:14 Umemwungama BWANA leo, kuwa ndiye Mungu wako, na kuwa yakupasa kutembea katika njia zake, na kushika amri zake na maagizo yake, na hukumu zake, na kusikiza sauti yake; 18#Kut 6:7; 19:5; Kum 4:20; 7:6; 14:2; 28:9; 2 Sam 7:23,24; Tit 2:14; 1 Pet 2:9 naye BWANA amekuungama hivi leo kuwa taifa iliyotengwa iwe yake yeye, kama alivyokuahidi, na kuwa yakupasa kushika maagizo yake yote; 19#Kum 4:7,8; 28:1; Zab 148:14; Kut 19:6; Law 20:24,26; Kum 7:6; 28:9; Zab 50:5; Isa 62:12; Yer 2:3; 1 The 5:27; 1 Pet 2:9 na kuwa atakutukuza juu ya mataifa yote aliyoyafanya, kwa sifa, na jina, na heshima, nawe upate kuwa taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako, kama alivyosema.
Iliyochaguliwa sasa
Kumbukumbu la Torati 26: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.