Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu la Torati 5

5
Amri kumi
1Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu nisemazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuzizingatia. 2#Kut 19:5; 24:7,8; Kum 4:23; Ebr 8:6-13; 9:19-23 BWANA, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu. 3#Mt 13:17; Ebr 8:9 BWANA hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai. 4#Kut 19:9,19; 20:22; Kum 4:33,36; 34:10 BWANA alisema nanyi uso kwa uso mlimani, kutoka kati ya moto; 5#Kut 19:16; 20:21; Hes 16:48; Zab 106:23; Yer 30:21; Gal 3:19; Ebr 12:18,19; Kut 24:2 (nami wakati ule nikiwa nimesimama kati ya BWANA na ninyi, ili kuwaonesha neno la BWANA; maana, mliogopa kwa sababu ya ule moto, wala hamkupanda mlimani); naye akasema, 6#Kut 20:2; Law 26:1; Kum 6:4; Zab 81:10 Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
7 # Kut 20:3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
8 # Law 26:1; Kum 4:15-18; 27:15; Kut 20:4; Zab 97:7; Mdo 17:29 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi. 9#Kut 34:6-7; Hes 14:18; Kum 7:9-10 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 10#Yer 32:18; Dan 9:4; 1 Yoh 1:7 nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
11 # Law 19:12; Kut 20:7; Yak 5:12; Mt 5:33 Usilitaje bure Jina la BWANA, Mungu wako; maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia, mtu alitajaye jina lake bure.
12 # Kut 16:23-30; 31:12-14; Kut 20:8; Neh 10:28-29 Ishike siku ya Sabato uitakase, kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru. 13#Kut 23:12; 31:15; 34:21; 35:2; Law 23:3; Eze 20:12 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 14#Mwa 2:2; Kut 16:29; Ebr 4:4 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng'ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe. 15Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.
16 # Kum 27:16; Mt 15:4; 19:19; Mk 7:10; 10:19; Lk 18:20; Efe 6:2,3; Law 19:3; Kol 3:20; Kum 4:40 Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
17 # Mwa 9:6; Law 24:17; Mt 5:21; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11 Usiue.
18 # Law 20:10; Mt 5:27; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11 Wala usizini.
19 # Law 19:11; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9 Wala usiibe.
20 # Kut 23:1; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; 1 Fal 21:10 Wala usimshuhudie jirani yako uongo.
21 # Rum 7:7; 13:9; Mik 2:2; Hab 2:9; Lk 12:15; Gal 5:14 Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu chochote alicho nacho jirani yako.
Musa mwakilishi wa mapenzi ya Mungu
22 # Ebr 12:18-19; Kut 24:12 Haya ndiyo maneno ambayo BWANA aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa. 23Ikawa, mlipoisikia sauti ile toka kati ya giza, na wakati uo huo mlima ule ulikuwa ukiwaka moto, basi, mlinikaribia, naam, wakuu wote wa makabila yenu, na wazee wenu, 24mkasema, Tazama, BWANA, Mungu wetu, ametuonesha utukufu wake, na ukuu wake, nasi tunasikia sauti yake toka kati ya moto; mmeona leo ya kuwa Mungu husema na mwanadamu, naye akaishi. 25Sasa basi, mbona tufe? Maana moto huu mkubwa utatuteketeza; tukiisikia tena sauti ya BWANA, Mungu wetu, tutakufa. 26#Kum 4:33 Maana katika watu wote ni nani aliyeisikia sauti ya Mungu aliye hai, akisema toka kati ya moto, kama vile sisi, asife? 27#Ebr 12:19 Nenda karibu wewe, ukasikie yote atakayoyasema BWANA, Mungu wetu; ukatuambie yote atakayokuambia BWANA, Mungu wetu; nasi tutayasikia na kuyatenda. 28Naye BWANA akasikia sauti ya maneno yenu mliyoniambia; BWANA akaniambia, Nimesikia sauti ya maneno ya watu hawa waliyokuambia; wamesema vema yote waliyosema. 29#Kum 32:29; Zab 81:13; Isa 48:18; Yer 44:4; Mt 23:37; Lk 19:42; 2 Kor 5:20; 6:1; 7:1; Ebr 12:25; Kum 11:1; Zab 119:1-5; Lk 11:28; Yn 15:14; Ufu 22:14 Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao sikuzote, wa kunicha, na kushika amri zangu zote sikuzote, wapate kufanikiwa wao na watoto wao milele! 30Enda uwaambie, Rudini hemani mwenu. 31#Mal 4:4; Gal 3:19 Lakini wewe, simama hapa karibu nami, nami nitasema nawe sheria zote, na amri na hukumu, utakazowafunza, wapate kuzifanya katika nchi niwapayo kuimiliki. 32#Kum 17:20; 28:14; Yos 1:7; 23:6; Mit 4:27 Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na BWANA, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kulia wala wa kushoto. 33#Kum 10:12; Zab 119:6; Mhu 8:12; Yer 7:23; Lk 1:6; 1 Tim 4:8; Kum 4:40; 12:25,28; 22:7; Efe 6:3 Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.

Iliyochaguliwa sasa

Kumbukumbu la Torati 5: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia