Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 1

1
1 # Mwa 32:28; 46:8-27; Kut 6:14 Basi majina ya wana wa Israeli walioingia Misri ni haya; kila mtu pamoja na jamaa zake walikuja pamoja na Yakobo. 2Reubeni, na Simeoni na Lawi, na Yuda; 3na Isakari, na Zabuloni, na Benyamini; 4na Dani, na Naftali, na Gadi, na Asheri. 5#Mwa 46:26; Kum 10:22 Na wale watu wote waliotokana na uzao wa Yakobo walikuwa watu sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo. 6#Mwa 50:26; Mdo 7:15; Mhu 1:4 Yusufu akafa, na ndugu zake wote, na watu wote wa kizazi kile. 7#Mdo 7:17; Mwa 46:3; Kum 26:5; Zab 105:24 Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.
Waisraeli wateswa
8 # Mdo 7:18 Basi akatokea mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. 9#Zab 105:24 Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. 10#Mdo 7:19; Zab 10:2; 83:3; Ayu 5:13; Mit 28:16 Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii. 11#Mwa 15:1; Kut 2:11; 3:7; 5:4; Mit 27:3; Zab 81:6; Mwa 47:11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. 12Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Ndipo Wamisri wakaogopa kwa sababu ya wana wa Israeli. 13Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; 14#Kut 2:23; 22:21; Law 25:14,17; Hes 20:15; Ayu 20:19; Mit 14:31; 22:22; Mdo 7:19,34; Zab 10:17,18; 81:6 wakafanya maisha yao kuwa machungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.
15Kisha mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; 16akasema, Wakati mnapowazalisha wanawake wa Kiebrania na kuona kuwa ni mtoto wa kiume basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto wa kike, na aishi. 17#Mit 16:6; Dan 3:16,18; 6:13; Mdo 5:29 Lakini hao wakunga walikuwa wacha Mungu, hawakufanya kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale watoto wa kiume. 18Basi mfalme wa Misri akawaita wale wakunga na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili la kuwahifadhi watoto wa kiume wawe hai? 19#Yos 2:4; 2 Sam 17:19,20 Wakunga wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mkunga hajapata kuwafikia. 20#Mit 11:18; Mhu 8:12; Isa 3:10; Ebr 6:10 Basi Mungu akawatendea mema wale wakunga; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi. 21#1 Sam 2:25; 2 Sam 7:11,13,27,29; 1 Fal 2:24; 11:38; Zab 127:1 Ilikuwa kwa sababu wale wakunga walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba. 22#Mdo 7:19 Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake wote, akisema, Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto wa kike mtamhifadhi hai.

Iliyochaguliwa sasa

Kutoka 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia