Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 19

19
Kushushwa kwa Israeli
1 # Eze 26:17 Tena uwaombolezee wakuu wa Israeli, 2useme, Mama yako alikuwa nini? Simba mke; alijilaza kati ya simba, kati ya wanasimba aliwalisha watoto wake. 3#2 Fal 23:31 Akamlea mtoto mmoja katika watoto wake, akawa mwanasimba, akajifunza kuwinda mawindo, akala watu. 4#2 Fal 23:33; 2 Nya 36:4; Yer 22:11 Mataifa nao wakapata habari zake, akanaswa katika rima lao, wakamchukua kwa kulabu mpaka nchi ya Misri. 5#2 Fal 23:34 Basi mamaye alipoona kwamba amemngoja, na tumaini lake limepotea, akatwaa mtoto mwingine katika watoto wake, akamfanya mwanasimba. 6#Yer 22:13 Naye akaenda huku na huko kati ya simba, akawa mwanasimba, akajifunza kuwinda mawindo, akala watu. 7Akayajua majumba yao, akaiharibu miji yao; nchi ikawa ukiwa, na vyote vilivyomo, kwa sababu ya mshindo wa kunguruma kwake. 8#2 Fal 24:2 Ndipo mataifa wakajipanga juu yake pande zote toka nchi zote; wakaunda wavu wao juu yake; akanaswa katika rima lao. 9#2 Nya 36:6; Yer 28:14; Eze 6:2 Wakamtia katika tundu kwa kulabu, wakamleta kwa mfalme wa Babeli wakamtia ndani ya ngome, sauti yake isisikiwe tena juu ya milima ya Israeli.
10 # Eze 15:2; Zab 80:8; Kum 8:7 Mama yako alikuwa kama mzabibu, katika damu yako, uliopandwa karibu na maji; akazaa sana na kujaa matawi, kwa sababu ya maji mengi. 11#Dan 4:11 Naye alikuwa na vijiti vya nguvu, kwa fimbo za enzi zao watawalao, na kimo chao kiliinuka kati ya matawi manene, wakaonekana kwa urefu wao, pamoja na wingi wa matawi yao. 12#Hos 13:15 Lakini aling'olewa kwa ghadhabu, akaangushwa chini, upepo wa mashariki ukakausha matunda yake; vijiti vyake vya nguvu vikavunjika, vikakauka; moto ulivila. 13#Kum 28:48 Na sasa umepandwa jangwani, katika nchi kavu, ya ukame. 14#Amu 9:15 Na moto umetoka katika vijiti vya matawi yake, umekula matunda yake, hata hana tena kijiti cha nguvu kifaacho kwa fimbo ya enzi ya kutawala. Na hayo ni maombolezo, nayo yatakuwa maombolezo.

Iliyochaguliwa sasa

Ezekieli 19: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia