Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 34

34
Dina abakwa
1 # Mwa 30:21; Tit 2:5 Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona binti za nchi. 2#Mwa 6:2; Amu 14:1 Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri. 3#Isa 40:2; Hos 2:14 Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri. 4#Amu 14:2 Shekemu akamwambia Hamori, babaye, akasema, Unipatie msichana huyu awe mke wangu. 5Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hadi walipokuja.
6Akatoka Hamori, babaye Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye. 7#Mwa 49:7; 2 Sam 13:12,21; Yos 7:15; Amu 20:6; Kum 23:17 Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka malishoni; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, jambo lisilostahili kutendeka. 8Hamori akasema nao, akinena, roho ya Shekemu, mwanangu, inamtamani binti yenu, tafadhalini, mpeni amwoe. 9#Kut 23:32 Mkaoane na sisi, mtupe sisi binti zenu, nanyi mkatwae binti zetu. 10#Mwa 13:9; 20:15; 42:34; 47:27 Nanyi mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo, mkapate mali humo. 11Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na nikubalike machoni penu, na mtakavyoniambia nitatoa. 12#Kut 22:16; Kum 22:29; 1 Sam 18:25 Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mke wangu.
13 # 2 Sam 13:24 Wana wa Yakobo wakawajibu Shekemu na Hamori babaye, kwa hila, maana amemharibu Dina, dada yao, 14#Yos 5:9 wakawaambia, Hatuwezi kufanya neno hili, tumpe dada yetu mtu asiyetahiriwa; ingekuwa aibu kwetu. 15Lakini kwa sharti hii tu tutapatana nanyi; mkiwa kama sisi, akitahiriwa kila mwanamume wenu, 16ndipo tutawapa ninyi binti yetu, na sisi tutatwaa binti zenu tutakaa pamoja nanyi, nasi tutakuwa watu wamoja. 17Lakini kama hamtusikii na kutahiriwa, basi tutamtwaa binti yetu, nasi tutakwenda zetu. 18Maneno yao yakawa mema machoni pa Hamori, na machoni pa Shekemu, mwana wa Hamori. 19#1 Nya 4:9 Na yule kijana hakukawia kulifanya neno lile, maana amependezewa na binti Yakobo, naye alikuwa mwenye heshima kuliko wote nyumbani mwa babaye.
20 # 2 Sam 15:2; Rut 4:1 Hamori, na Shekemu mwanawe, wakaja langoni pa mji wao, wakasema na watu wa mji wao, wakinena, 21Watu hawa wana amani nasi, basi na wakae katika nchi, na kufanya biashara humo; kwa maana nchi ni kubwa, yawatosha; na tuwatwae binti zao kuwa wake zetu, na binti zetu tuwape wao. 22Lakini kwa sharti hiyo moja tu watapatana nasi wakae wote kwetu, tuwe watu wamoja, kama tukitahiriwa kila mwanamume, kama wao walivyotahiriwa. 23Je! Kondoo zao, na mali zao, na wanyama wao wote hawatakuwa mali zetu? Basi na tupatane nao tu, nao watakaa kwetu. 24#Mwa 23:10 Wakawasikia Hamori na Shekemu mwanawe, wote watokeao katika lango la mji wake. Wakatahiriwa kila mwanamume, wote watokao katika lango la mji wake.
Ndugu zake Dina walipiza Kisasi
25 # Mwa 49:5-7 Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina, wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua wanaume wote. 26Wakawaua Hamori, na Shekemu mwanawe, kwa upanga, wakamtwaa Dina katika nyumba ya Shekemu, wakatoka.
27Wana wa Yakobo wakawajia hao waliouawa, wakaupora mji kwa sababu wamemharibu dada yao. 28Wakachukua kondoo wao, na ng'ombe wao, na punda wao, na vitu vilivyokuwamo mjini, na vile vilivyokuwako kondeni. 29Wakatwaa na mali yao zote, watoto wao wote, na wake zao wakateka na hata wakapora vyote vilivyokuwemo nyumbani. 30#Mwa 49:6; Yos 7:25; Kut 5:21; 1 Sam 13:4; Kum 4:27; Zab 105:12 Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, Mmenitaabisha, kunifanya ninuke vibaya kati ya watu wa nchi hii, Wakanaani na Waperizi; na mimi, kwa kuwa watu wangu ni haba, watanikusanyikia, na kunipiga, nami nitaangamizwa, mimi na nyumba yangu. 31Nao wakasema, Je! Ni vema amtendee dada yetu kama kahaba?

Iliyochaguliwa sasa

Mwanzo 34: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia