Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 35

35
Yakobo arudi Betheli
1 # Mwa 28:11-17,19; 27:43; 28:13 Mungu akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako.
2 # Mwa 31:19; Yos 24:15; 1 Sam 7:3; Kut 19:10 Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu. 3#Mwa 32:7,24; Zab 107:6; Mwa 28:20; 31:3,42 Tuondoke, tupande kwenda Betheli, nami nitamfanyia Mungu madhabahu huko; yeye aliyenisikia siku ya shida yangu, akawa pamoja nami katika njia yote niliyoiendea. 4#Hos 2:13; Yos 24:26 Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na vipuli vilivyokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu. 5#Kut 15:16; 23:27; Kum 11:25; Yos 2:9; 5:1; 2 Nya 14:14 Wakashika njia, hofu ya Mungu ikaishika miji iliyowazunguka, wala hawakuwafuata wana wa Yakobo.
6 # Mwa 28:22 Basi Yakobo akafika Luzu, katika nchi ya Kanaani, ndio Betheli, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye. 7#Mhu 5:4; Mwa 28:13 Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake. 8#Mwa 24:59 Akafa Debora mlezi wa Rebeka, akazikwa chini ya Betheli, chini ya mwaloni; na jina lake likaitwa Alon-bakuthi.#35:8 Alon-bakuthi: maana yake ni Mwaloni wa Vilio.
9 # Hos 12:4 Mungu akamtokea Yakobo tena, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki. 10#Mwa 17:5; 32:28 Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli. 11#Mwa 17:4-8; 48:3,4; Kut 6:3 Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka katika uzao wako.#35:11 Katika Kiebrania ni viunoni mwako. 12#Mwa 12:7; 13:15; 28:13; Kut 32:13 Na nchi hii niliyowapa Abrahamu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo. 13#Mwa 17:22 Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye. 14#Mwa 28:18-19 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake. 15Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.
Kuzaliwa kwa Benyamini na kufa kwa Raheli
16Wakasafiri kutoka Betheli, na kabla ya kufika Efrata, Raheli akashikwa na uchungu wa kuzaa, na uchungu wake ulikuwa mkali. 17#Mwa 30:24 Ikawa alipokuwa anashikwa sana na uchungu, mkunga akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine. 18Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini. 19#Mwa 48:7; Rut 1:2; 4:11; Mik 5:2; Mt 2:6 Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu. 20#1 Sam 10:2 Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo. 21#Mik 4:8 Kisha akasafiri Israeli akapiga hema yake upande wa pili wa mnara wa Ederi. 22#Mwa 49:4; 1 Nya 5:1 Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari.
Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili. 23#Mwa 46:8; Kut 1:2 Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni. 24Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini. 25Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali. 26Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu.
Kufa kwa Isaka
27 # Mwa 13:18; Yos 14:15 Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Abrahamu na Isaka. 28Siku za Isaka zilikuwa miaka mia moja na themanini. 29#Mhu 12:7; Mwa 15:15; 25:8,9; 49:31 Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.

Iliyochaguliwa sasa

Mwanzo 35: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia