Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 36

36
Wazawa wa Esau
1 # Mwa 25:30 Hivi ndivyo vizazi vya Esau, ndiye Edomu. 2#Mwa 26:34 Esau alitwaa binti za Kanaani, kuwa wakeze; Ada, binti Eloni, Mhiti, na Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, Mhivi; 3#Mwa 28:9 na Basemathi, binti Ishmaeli, nduguye Nebayothi. 4#1 Nya 1:35 Ada akamzalia Esau Elifazi; na Basemathi alizaa Reueli. 5Oholibama alizaa Yeushi, na Yalamu, na Kora. Hao ndio wana wa Esau aliozaliwa katika nchi ya Kanaani.
6 # Kum 23:7 Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng'ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye. 7#Mwa 13:6,11; 17:8; 1 Nya 29:15; Zab 39:12; 105:12; Ebr 11:9; 1 Pet 1:17; 2:11 Maana mali yao ilikuwa nyingi wasiweze kukaa pamoja, wala nchi ya ugeni haikuweza kuwapokea kwa sababu ya wingi wa mifugo wao.
8 # Mwa 32:3 Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu. 9Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri. 10#1 Nya 1:35 Haya ndiyo majina ya wana wa Esau; Elifazi, mwana wa Ada mkewe Esau. Reueli, mwana wa Basemathi, mkewe Esau. 11Na wana wa Elifazi, ni Temani na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi. 12#Kut 17:8; Hes 24:20; Kum 25:17-19; 1 Sam 15:2,3 Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau.
13Na hawa ni wana wa Reueli: Nahathi, na Zera, na Shama na Miza. Hao walikuwa wana wa Basemathi, mkewe Esau.
14Na hawa ni wana wa Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, mkewe Esau; akamzalia Esau, Yeushi, na Yalamu, na Kora.
Watawala wa Edomu
15Hawa ndio majumbe wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; jumbe Temani, jumbe Omari, jumbe Sefo, jumbe Kenazi, 16jumbe Kora, jumbe Gatamu, jumbe Amaleki. Hao ndio majumbe, waliotoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Ada.
17Na hawa ni wana wa Reueli, mwanawe Esau; jumbe Nahathi, jumbe Zera, jumbe Shama, jumbe Miza. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Basemathi, mkewe Esau.
18Na hawa ni wana wa Oholibama, mkewe Esau; jumbe Yeushi, jumbe Yalamu, jumbe Kora. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Oholibama, binti Ana, mkewe Esau.
19Hao ni wana wa Esau, na hao ndio majumbe wao; naye Esau ndiye Edomu.
20 # 1 Nya 1:38; Mwa 14:6; Kum 2:12,22 Hawa ni wana wa Seiri, Mhori, wenyeji wa nchi ile; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, 21na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, wana wa Seiri, katika nchi ya Edomu.
22Na wana wa Lotani, ni Hori, na Hemamu; na dada yake Lotani ni Timna. 23Na hawa ni wana wa Shobali, Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. 24#Law 19:19 Na hawa ni wana wa Sibeoni, Aya, na Ana; ni yule Ana aliyeona chemchemi za maji ya moto katika jangwa, alipokuwa akichunga punda za Sibeoni babaye. 25Na hawa ni wana wa Ana, Dishoni, na Oholibama, binti Ana. 26Na hawa ni wana wa Dishoni, Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. 27Na hawa ni wana wa Eseri, Bilhani, na Zaawani, na Akani. 28Na hawa ni wana wa Dishani, Usi, na Arani.
29Hawa ndio majumbe waliotoka katika Wahori; jumbe Lotani, jumbe Shobali, jumbe Sibeoni, jumbe Ana, 30jumbe Dishoni, jumbe Eseri jumbe Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, kwa habari za majumbe yao, katika nchi ya Seiri.
31 # 1 Nya 1:43; 1 Sam 10:24 Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli. 32Bela wa Beori alimiliki katika Edomu, na jina la mji wake ni Dinhaba. 33Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake. 34Akafa Yobabu, akamiliki Hushamu, wa nchi ya Watemani, badala yake. 35Akafa Hushamu, akamiliki Hadadi wa Bedadi badala yake, naye ndiye aliyepiga Midiani katika nyika ya Moabu, na jina la mji wake ni Avithi. 36Akafa Hadadi, akamiliki Samla wa Masreka badala yake. 37Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake. 38Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake. 39#1 Nya 1:50 Akafa Baal-hanani, mwana wa Akbori, akamiliki Hadadi badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu.
40 # 1 Nya 1:51 Na hayo ndiyo majina ya majumbe waliotoka kwa Esau, kufuata jamaa zao, na mahali pao, kwa majina yao. Jumbe Timna, jumbe Alva, jumbe Yethethi, 41jumbe Oholibama, jumbe Ela, jumbe Pinoni, 42jumbe Kenazi, jumbe Temani, jumbe Mibsari, 43jumbe Magdieli, jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu, kulingana na makao yao, katika nchi ya mamlaka yao. Naye huyo ndiye Esau, baba ya Edomu.

Iliyochaguliwa sasa

Mwanzo 36: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia