Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waraka kwa Waebrania 7:11-17

Waraka kwa Waebrania 7:11-17 SRUV

Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine awepo, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni? Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike. Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kabila nyingine, ambayo hapana mtu wa kabila hilo aliyeihudumia madhabahu. Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambalo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani. Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine kama Melkizedeki; asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na kikomo; maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Waraka kwa Waebrania 7:11-17