Hosea 6
6
Mwito wa toba
1 #
Ayu 5:18; Kut 15:26; Isa 30:26; Yer 30:17; Eze 34:16 Njooni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga majeraha yetu. 2Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. 3#Mit 2:1-9; Mt 13:11; Ayu 29:23 Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.
Uovu wa Israeli na Yuda
4Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema. 5#Yer 1:10; Ebr 4:12 Kwa sababu hiyo nimewakatakata kwa vinywa vya manabii; nimewaua kwa maneno ya kinywa changu; na hukumu yangu itatokea kama mwanga. 6#Mit 21:3; Zab 50:8; Yn 17:3; Mt 9:13; 12:7 Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa. 7Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana. 8Gileadi ni mji wa hao watendao maovu, umetiwa rangi ya damu. 9Na kama vile makundi ya wanyang'anyi wamwoteavyo mtu, ndivyo kundi la makuhani wauavyo katika njia ielekeayo Shekemu; naam, wametenda mambo maovu sana. 10Katika nyumba ya Israeli nimeona jambo bovu kabisa; huko uzinzi umeonekana katika Efraimu; Israeli ametiwa unajisi. 11#Zab 126:1 Tena, Ee Yuda, wewe umeandikiwa mavuno, hapo nitakapowarudisha wafungwa wa watu wangu.
Iliyochaguliwa sasa
Hosea 6: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.