Isaya 63
63
Kisasi juu ya Edomu
1 #
Isa 34:5-17; Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; 35:1-15; Amo 1:11-12; Oba 1-14; Mal 1:2-5 Ni nani huyu atokaye Edomu,
Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu?
Huyu aliye na nguo za fahari,
Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake?
Ndimi nisemaye kwa haki,
Niliye hodari wa kuokoa.
2 #
Ufu 19:13
Kwa nini mavazi yako ni mekundu,
Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu?
3 #
Omb 1:15; Mal 4:3; Ufu 14:20; 19:13,15 Nilikanyaga shinikizoni peke yangu;
Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami;
Naam, niliwakanyaga kwa hasira yangu,
Niliwaponda kwa ghadhabu yangu;
Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao,
Nami nimezichafua nguo zangu zote.
4Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu,
Na mwaka wao niliowakomboa umewadia.
5 #
Yn 16:32; Zab 44:3; 98:1; Isa 40:10; 51:9; Isa 59:16 Nikatazama, wala hapakuwa na wa kunisaidia;
Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza;
Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu,
Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.
6 #
Ufu 16:6
Nikayakanyaga makabila ya watu kwa hasira yangu,
Nikawalevya kwa ghadhabu yangu,
Nami nikaimwaga damu yao chini.
Rehema za Mungu zakumbukwa
7Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake. 8Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao. 9#Mdo 9:4; 12:11; Kut 14:19; Hos 12:4,5; Mal 3:1; Kum 7:7 Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale. 10#Zab 78:8,40; Mdo 7:51; Efe 4:30; Ebr 10:29 Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao. 11Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu? 12#Kut 14:21 Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu, kwa mkono wa kulia wa Musa? Aliyeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele? 13Aliyewaongoza vilindini, kama farasi jangwani, wasijikwae? 14Kama ng'ombe washukao bondeni, Roho ya BWANA ikawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu.
Sala ya toba
15Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu. 16#Gal 3:28 Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Abrahamu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, BWANA, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako. 17#Zab 119:10; Isa 6:10; Mt 13:15 Ee BWANA, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanya kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, makabila ya urithi wako. 18#Dan 8:24 Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako. 19Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako.
Iliyochaguliwa sasa
Isaya 63: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.