Waamuzi 2
2
Kutotii kwa Israeli
1 #
Mwa 16:7; 32:11; Kut 3:1-6; Yn 1:1; 7:5-8; Mwa 17:7; Kut 6:4; Zab 105:8-11; Mik 7:20; Lk 1:54,55,72-75 Kisha malaika wa BWANA alikwea kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hadi nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi; 2#Kut 34:12-13; Kum 7:2-5 nanyi msifanye agano lolote na hawa wenyeji wa nchi hii; yabomoeni madhabahu yao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani? 3#Yos 23:13; Kut 23:33; 34:12; Kum 7:16; Amu 3:6; Zab 106:36 Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni mtego kwenu. 4Ikawa, hapo huyo malaika wa BWANA alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia. 5Nao wakaliita jina la mahali pale Bokimu;#2:5 Katika Kiebrania ni ‘Wanaolia’. nao wakamchinjia BWANA sadaka huko.
Kifo cha Yoshua
6Basi hapo Yoshua alipowapa watu ruhusa waende zao, wana wa Israeli wakaenda kila mtu kuuendea urithi wake, ili kuimiliki hiyo nchi. 7Watu hao wakamtumikia BWANA siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioendelea siku zao baada ya Yoshua, hao waliokuwa wameiona hiyo kazi kubwa ya BWANA yote, aliyokuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli. 8Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa, naye alikuwa na umri wa miaka mia moja na kumi. 9#Yos 19:49-50 Nao wakamzika katika mpaka wa urithi wake katika Timnath-heresi, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi. 10#Kut 5:2; 1 Sam 2:12; 1 Nya 28:9; Yer 9:3; 22:16; Gal 4:8; 2 The 1:8; Tit 1:16 Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua BWANA, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.
Uasi wa Israeli
11Wana wa Israeli walifanya mambo maovu mbele za macho ya BWANA, na wakawatumikia Mabaali. 12#Kum 13:5; 31:16; Yos 24:20; Amu 10:6,13; 1 Nya 28:9; Kum 6:14; Yer 2:11,13; Kut 20:5 Wakamwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha BWANA, akaghadhibika. 13Wakamwacha BWANA, wakamtumikia Baali na Maashtorethi. 14#Amu 3:8; 2 Nya 7:19; Zab 78:58-62; 106:40; Isa 1:28; 2 Fal 17:20; Amu 3:8; 4:2; Zab 44:12; Isa 50:1; Law 26:37; Yos 7:12 Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao. 15#Law 26:14,34; Kum 28:15-68 Kila walikokwenda mkono wa BWANA ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama BWANA alivyosema, na kama BWANA alivyowaapia; nao wakafadhaika sana. 16#Amu 3:9; 1 Sam 12:11; Mdo 13:20 Kisha BWANA akawainua waamuzi, waliowaokoa mikononi mwa watu hao waliowateka nyara. 17#Kut 34:15,16; Law 17:7; Ufu 17:1-5 Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za BWANA bali wao hawakufanya hivyo. 18#Yos 1:5; Mwa 6:6; Kum 32:36; Zab 106:44; Yer 18:7-10; Yon 3:10 Na kila wakati BWANA alipowainulia waamuzi, ndipo BWANA alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana BWANA alisikitishwa na kilio chao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua. 19Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi.
20 #
Yos 23:16
Basi hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akasema, Kwa kuwa taifa hili limelivunja agano langu nililowaamuru baba zao, wala hawakuisikiliza sauti yangu; 21mimi nami tokea sasa sitalifukuza taifa mojawapo la hayo aliyoyaacha Yoshua alipokufa; 22#Kum 8:2; 13:3 ili kwa njia ya hayo nipate kuwajaribu Israeli, kama wataifuata njia ya BWANA kwenda katika njia hiyo, au sivyo. 23Basi BWANA akawaacha mataifa yale, wala hakuwafukuza kwa upesi, wala hakuwatia katika mikono ya Yoshua.
Iliyochaguliwa sasa
Waamuzi 2: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.