Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 37

37
Tumaini la bure la Sedekia
1 # 1 Nya 3:16; Dan 1:1; 2 Fal 24:17; 2 Nya 36:10 Na Sedekia, mwana wa Yosia, akamiliki baada ya Konia, mwana wa Yehoyakimu, ambaye Nebukadneza amemfanya mtawala katika nchi ya Yuda. 2#2 Fal 24:19,20; Mit 29:12 Lakini yeye, wala watumishi wake, wala watu wa nchi, hawakuyasikiliza maneno ya BWANA aliyonena kwa kinywa cha nabii Yeremia.
3 # Yer 21:1,2 Sedekia, mfalme, akamtuma Yehukali, mwana wa Shelemia, na Sefania, mwana wa Maaseya, kuhani, kwa Yeremia, nabii, kusema, Utuombee sasa kwa BWANA, Mungu wetu. 4Basi Yeremia alikuwa akiingia na kutoka kati ya watu; kwa maana walikuwa hawajamfunga gerezani. 5#2 Fal 24:7; Yer 34:21 Na jeshi la Farao lilikuwa limetoka nchi ya Misri; na Wakaldayo waliohusuru Yerusalemu, waliposikia habari zao, wakavunja kambi yao mbele ya Yerusalemu. 6Ndipo neno la BWANA likamjia nabii Yeremia, kusema, 7#Yer 21:2 BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; Mtamwambia hivi mfalme wa Yuda, aliyewatuma kwangu kuniuliza; Angalieni, jeshi la Farao, ambalo linakuja kuwasaidia, litarudi Misri, nchi yao wenyewe. 8#Zab 33:10; Mit 21:30; Isa 30:1-7; Yer 34:22 Na Wakaldayo watakuja tena, na kupigana na mji huu; nao watautwaa, na kuuteketeza. 9BWANA asema hivi, Msijidanganye mkisema, Bila shaka Wakaldayo watatuacha na kwenda zao; maana hawatawaacha. 10#Law 26:36-38; Isa 30:17; Yer 21:4,5 Maana mngelipiga jeshi lote la Wakaldayo wanaopigana nanyi, wakabaki kati yao watu waliojeruhiwa tu, hata hivyo wangeondoka kila mtu katika hema yake, na kuuteketeza mji huu.
Yeremia atiwa gerezani
11Hata ikawa, jeshi la Wakaldayo lilipokuwa limevunja kambi yao mbele ya Yerusalemu, kwa kuliogopa jeshi la Farao, 12ndipo Yeremia akatoka Yerusalemu, ili aende mpaka katika nchi ya Benyamini, alipokee huko fungu lake kati ya watu. 13Naye alipokuwa katika lango la Benyamini, mkuu wa walinzi alikuwapo, jina lake Iriya, mwana wa Shelemia, mwana wa Hanania; akamkamata Yeremia, nabii, akisema, Unakwenda kujiunga na Wakaldayo. 14Ndipo Yeremia akasema, Ni uongo, siendi kujiunga na Wakaldayo; lakini yeye asimwamini; basi Iriya akamkamata Yeremia, akamleta kwa wakuu. 15#Yer 20:1-3; Mt 21:35; Yn 18:22; Mdo 5:40; Mwa 30:20; Yer 38:26; Mdo 12:6; Ufu 2:10 Nao wakuu wakamkasirikia Yeremia, wakampiga, wakamtia gerezani katika nyumba ya Yonathani, mwandishi; kwa maana ndiyo waliyoifanya kuwa gereza. 16#Yer 38:6 Basi, Yeremia alipokuwa ameingia katika nyumba ya shimo, na katika vyumba vya ndani; na Yeremia alipokuwa amekaa humo siku nyingi; 17#Mk 6:20 ndipo Sedekia, mfalme, akatuma watu wamlete; naye mfalme akamwuliza kwa siri ndani ya nyumba yake, akasema, Je! Liko neno lililotoka kwa BWANA? Yeremia akasema, Liko. Akasema pia, Utatiwa katika mikono ya mfalme wa Babeli. 18Pamoja na haya Yeremia akamwambia mfalme Sedekia, Nimefanya kosa gani juu yako, au juu ya watumishi wako, au juu ya watu hawa, hata mkanitia gerezani? 19Wako wapi sasa manabii wenu waliowatabiria, wakisema, Mfalme wa Babeli hatakuja juu yenu, wala juu ya nchi hii? 20Na sasa unisikilize, Ee bwana wangu mfalme; maombi yangu yakapate kibali mbele yako; usinirudishe nyumbani mwa Yonathani, mwandishi, nisije nikafa humo. 21#Yer 32:2; 1 Fal 17:6,9; 2 Fal 25:3; Yer 38:9; 2 Kor 6:4 Ndipo Sedekia mfalme akatoa amri, wakamtia Yeremia katika ukumbi wa walinzi; wakampa kila siku mkate mmoja uliotoka katika njia ya waokaji, hata mkate wote wa mji ulipokwisha. Basi Yeremia akakaa katika ukumbi wa walinzi.

Iliyochaguliwa sasa

Yeremia 37: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia