Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 10

10
Nayachukia maisha yangu
1Nayachukia maisha yangu;
Nitayasema malalamiko yangu wazi;
Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.
2Nitamwambia Mungu, Usinihukumie makosa;
Nijulishe kwa nini unapingana nami.
3Je! Ni vema kwako wewe kuonea,
Na kuidharau kazi ya mikono yako,
Na kuiunga mkono mipango ya waovu?
4 # 1 Sam 16:7; Lk 16:15; Ufu 1:14 Je! Wewe una macho ya kimwili,
Au je! Waona kama aonavyo binadamu?
5Je! Siku zako ni kama siku za mtu,
Au je! Miaka yako ni kama miaka ya mtu,
6Hata ukaulizauliza habari za uovu wangu,
Na kuitafuta dhambi yangu,
7Ujapojua ya kuwa mimi si mwovu;
Wala hapana awezaye kuokoa kutoka kwa mkono wako?
8 # Zab 119:73; Isa 43:7 Mikono yako imeniumba na kunifinyanga;
Nawe utageuka na kuniangamiza?
9 # Mwa 2:7; Isa 45:9 Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo;
Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
10 # Zab 139:14 Je! Wewe hukunimimina kama maziwa,
Na kunigandisha mfano wa jibini?
11Umenivika ngozi na nyama,
Na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa.
12Unanijalia uhai na fadhili,
Na kwa uangalifu wako roho yangu imetunzwa.
13Lakini mambo haya uliyaficha moyoni mwako;
Najua kuwa haya yamo nafsini mwako;
14Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia,
Wala hutaniachilia na uovu wangu.
15 # Zab 9:17; Isa 3:11; Mal 3:18; Ayu 9:12; Kut 3:7; Zab 25:18; Omb 1:20 Mimi nikiwa mwovu, ole wangu!
Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu;
Maana nimejaa aibu
Nikiyaangalia mateso yangu.
16 # Isa 38:13; Omb 3:10 Kichwa changu kikijiinua, waniwinda kama simba;
Tena wajionesha kwangu kuwa wa ajabu.
17Wewe unafanya upya ushahidi wako juu yangu,
Na kuongeza kisirani chako juu yangu;
Ukileta jeshi baada ya jeshi juu yangu.
18Kwa nini basi kunitoa tumboni?
Ningekata roho, lisinione jicho lolote.
19Ningalikuwa kama mtu asiyekuwapo;
Ningalichukuliwa kaburini kutoka tumboni.
20 # Zab 39:13; Ayu 7:16 Je! Siku zangu si chache? Acha basi,
Usinisumbue, nipate angaa kutulizwa moyo kidogo.
21 # Ayu 3:5; Zab 88:12; 23:4 Kabla sijaenda huko ambako sitarudi kutoka huko tena,
Ni hiyo nchi ya giza, giza tupu;
22Ni nchi ya giza kuu, kama giza lenyewe lilivyo;
Ni nchi ya giza tupu, isiyo na mpango wowote wa mambo,
Nchi ambayo nuru yake ni kama giza.

Iliyochaguliwa sasa

Ayubu 10: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia