Ayubu 42
42
Ayubu anyenyekezwa na kutoshelezwa
1Ndipo Ayubu akamjibu BWANA, na kusema.
2 #
Yer 32:17; Mt 3:9; Mk 14:36; Lk 1:37; Efe 3:20 Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote,
Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.
3 #
Ayu 38:2; 1 Tim 1:7; Zab 40:5 Ni nani huyu afichaye ushauri bila maarifa?
Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu,
Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua.
4 #
Ayu 38:3
Sikiliza, nakusihi, nami nitanena;
Nitakuuliza neno, nawe niambie.
5 #
Rum 10:17; Hes 12:8,9; Isa 6:1 Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio;
Bali sasa jicho langu linakuona.
6Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu
Katika mavumbi na majivu.
Marafiki wa Ayubu waaibishwa
7Basi ikawa, baada ya BWANA kumwambia Ayubu maneno hayo, BWANA akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. 8#Hes 23:1; Ebr 10:4; Mt 5:24; Mwa 20:17; Ebr 7:25; Yak 5:16 Basi sasa, jitwalieni ng'ombe dume saba, na kondoo dume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende kulingana na upumbavu wenu; kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. 9Basi Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya kama vile BWANA alivyowaamuru; naye BWANA akamridhia Ayubu.
Ayubu arejeshewa mali yake maradufu
10 #
Ayu 1:1-3; Isa 40:2 Kisha BWANA akamrejeshea Ayubu mali yake, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza. 11#Ayu 19:13 Ndipo wakamwendea ndugu zake wote, wanaume kwa wanawake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakampa pole na kumliwaza kwa ajili ya mateso hayo yote aliyoleta BWANA juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja. 12#Ayu 8:7; 1:3 Basi hivyo BWANA akaubariki huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu moja, na punda wake elfu moja. 13Tena alikuwa na watoto wa kiume saba, na binti watatu. 14Akamwita huyo wa kwanza jina lake Yemima; na wa pili akamwita jina lake Kesia; na wa tatu akamwita jina lake Keren-hapuhu. 15Katika nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri kama hao wana wa Ayubu; na baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao wa kiume. 16#Ayu 5:26 Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia moja na arubaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hadi kizazi cha nne. 17#Mwa 25:8 Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana mwenye kujawa na siku.
Iliyochaguliwa sasa
Ayubu 42: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.