Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yona 2

2
Wimbo wa kushukuru
1Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, akiwa katika tumbo la yule samaki, 2Akasema,
Nilimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu,
Naye akaniitikia;
Katika tumbo la kuzimu niliomba,
Nawe ukasikia sauti yangu.
3 # Zab 88:6 Maana ulinitupa vilindini,
Ndani ya moyo wa bahari;
Gharika ya maji ikanizunguka pande zote;
Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.
4 # Zab 31:22; Isa 49:14; 1 Fal 8:38 Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako;
Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.
5Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu;
Vilindi vilinizunguka;
Mwani ulikizinga kichwa changu;
6Nilishuka hata pande za chini za milima;
Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele;
Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni,
Ee BWANA, Mungu wangu,
7 # Zab 18:6; 34:6; 130:2; Yer 2:13 Roho yangu ilipozimia ndani yangu,
Nilimkumbuka BWANA;
Maombi yangu yakakufikia,
Katika hekalu lako takatifu.
8 # 2 Fal 17:15; Zab 31:6; Yer 10:8 Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo
Hujitenga na rehema zao wenyewe.
9 # Zab 50:14; 66:13-15; Hos 14:2; Ebr 13:15 Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani;
Nitaziondoa nadhiri zangu.
Wokovu hutoka kwa BWANA.
10 # Yon 1:17; Mt 8:9 BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona katika pwani.

Iliyochaguliwa sasa

Yona 2: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia