Yoshua 8
8
Ai Watekwa kwa hila na kuangamizwa
1 #
Kum 1:21; 7:18; 31:8; Yos 1:9; 2:11; 6:2; Zab 44:3 Kisha BWANA akamwambia Yoshua, Usiogope, wala usifadhaike; wachukue wanajeshi wako wote waende pamoja nawe, nanyi inukeni, mwende Ai, angalia, mimi nimemtia mkononi mwako huyo mfalme wa Ai, na watu wake, na mji wake, na nchi yake; 2#Yos 6:21; Kum 20:14 nawe utautenda mji wa Ai na mfalme wake kama ulivyoutenda mji wa Yeriko na mfalme wake; lakini nyara zake na wanyama wake wa mji mtavitwaa kuwa mateka yenu wenyewe; huo mji uuwekee waoteaji upande wa nyuma. 3Basi Yoshua akainuka, na watu wote wa vita pamoja naye, ili waende Ai; Yoshua akachagua watu elfu thelathini, watu mashujaa wenye uwezo, akawatuma wakati wa usiku. 4#Amu 20:29; 2 Nya 13:13 Akawaagiza, akasema, Angalieni, mtaotea kuuvizia ule mji, upande wa nyuma wa mji; msiende mbali sana na mji, lakini kaeni tayari nyote; 5#Amu 20:32 na mimi, na watu wote walio pamoja nami, tutaukaribia mji; kisha itakuwa, hapo watakapotoka nje kupigana nasi, kama walivyofanya hapo kwanza, sisi tutakimbia mbele yao; 6nao watatoka nje watufuate, hadi tuwavute waende mbali na mji wao; kwa kuwa watasema, Wakimbia mbele yetu, kama walivyofanya kwanza; nasi tutakimbia mbele yao; 7basi ninyi mtainuka mtoke hapo mwoteapo, na kuushika mji; kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, atautia mikononi mwenu. 8#Yos 1:16; 2 Sam 13:28 Kisha itakuwa, mtakapoushika mji, ndipo mtauteketeza mji kwa moto; sawasawa na hilo neno la BWANA; angalieni, nimewaagiza. 9Basi Yoshua akawatuma; nao wakaenda hadi hapo watakapootea, wakakaa kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa Ai; lakini Yoshua akalala usiku huo kati ya watu.
10 #
Mwa 22:3; Yos 3:1; 6:12; 7:16; Zab 101:8; 119:60; Mhu 9:10; Yer 21:12 Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakutanisha watu, kisha akatangulia kukwea kwenda Ai mbele ya hao watu, yeye na wazee wa Israeli. 11Watu wote, hao wa vita, waliokuwa pamoja naye, wakaenda wakakaribia, na kufika mbele ya mji, wakatua upande wa kaskazini wa Ai; napo palikuwa na bonde kati yao na Ai. 12#Mwa 12:8; 28:19; Amu 1:22 Kisha akatwaa watu kama elfu tano, akawaweka kuotea kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa huo mji. 13Basi wakawaweka hao watu, jeshi zima lililokuwa upande wa kaskazini wa mji, na wale waliokuwa wakiotea upande wa magharibi wa mji; naye Yoshua akaenda usiku huo katikati ya hilo bonde. 14#Amu 20:34; Mhu 9:12; Mt 24:39,50; 1 The 5:1-3; 2 Pet 2:3 Kisha ikawa hapo huyo mfalme wa Ai alipoona jambo hilo, ndipo walipofanya haraka, na wakaamka asubuhi na mapema, na wanaume wa mji wakatoka nje waende kupigana na Israeli, yeye na watu wake wote, kwa wakati ulioamriwa, kuikabili Araba; lakini hakujua ya kwamba walikuwako waviziao kinyume chake kwa upande wa nyuma wa mji. 15#Amu 20:36; Yos 15:61; 16:1; 18:12 Kisha Yoshua na watu wa Israeli wote walifanya kana kwamba wameshindwa mbele yao, wakakimbia kwa njia ya nyika. 16#Kut 14:3,4; Zab 9:16; Amu 20:31 Watu wote waliokuwa ndani ya mji waliitwa wakusanyike pamoja ili kuwafuatia; nao wakamfuatia Yoshua, wakasongea mbele na kuuacha mji. 17Hakusalia mtu yeyote ndani ya Ai, au katika Betheli, asiyetoka nje kuwafuatia Israeli; wakauacha mji wazi na kuwafuatia Israeli. 18#Kum 7:23,24; 9:3; Yos 1:5; Yer 49:3 Kisha BWANA akamwambia Yoshua, Haya, unyoshe huo mkuki ulio nao mkononi mwako, uuelekeze upande wa Ai; kwa kuwa nitautia mkononi mwako. Basi Yoshua akaunyosha huo mkuki uliokuwa mkononi mwake kuuelekea huo mji. 19Wale watu waliovizia wakainuka upesi kutoka mahali pao, nao wakapiga mbio mara hapo alipokuwa amekwisha unyosha mkono wake, wakaingia ndani ya mji, na kuushika; nao wakafanya haraka kuuteketeza kwa moto huo mji.
20Kisha hapo hao watu wa Ai walipotazama nyuma yao, wakaona, na tazama, moshi wa huo mji ulikuwa unapaa juu kwenda mawinguni, nao hawakuwa na nguvu za kukimbia huku wala huku; na wale watu waliokuwa wamekimbia kwenda nyikani wakageuka na kuwarudia hao waliokuwa wakiwafuatia. 21Basi hapo Yoshua na Israeli wote walipoona ya kwamba hao waliovizia wamekwisha kuushika huo mji, na ya kwamba moshi wa mji umepaa juu, ndipo wakageuka tena, na kuwaua watu wa Ai. 22#Law 27:29; Kum 7:2; Ayu 20:5; Lk 17:26-30; 1 The 5:3 Tena hao; wengine wakatoka nje ya mji huo kinyume chao; hivyo basi wakawa katikati ya Waisraeli, wengine upande huu na wengine upande ule; nao wakawapiga, hata wasimwache hata mmoja miongoni mwao aliyesalia, wala kupona. 23Kisha wakamshika mfalme wa Ai akiwa hai, nao wakamleta kwa Yoshua. 24Kisha ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamekwisha kuwaua wenyeji wote wa Ai katika bara, hapo katika nyika walipokuwamo wakiwafuatia, nao walikuwa wamekwisha anguka wote kwa makali ya upanga, hadi walipokuwa wameangamizwa wote, ndipo Israeli wakarejea Ai, na kuupiga huo mji kwa makali ya upanga. 25Wote walioanguka siku hiyo wanaume kwa wanawake, walikuwa ni elfu kumi na mbili, yaani, watu wote wa mji wa Ai. 26Kwani huyo Yoshua hakuuzuia mkono wake, huo ulionyosha huo mkuki, hadi hapo alipokuwa amewaangamiza kabisa wenyeji wote wa Ai; 27#Hes 31:22,26; Mt 20:15 Isipokuwa mifugo na nyara za mji Israeli wakatwaa wenyewe kuwa ni mapato yao, sawasawa na hilo neno la BWANA alilomwamuru Yoshua. 28#Kum 13:16; 2 Fal 19:25; Isa 17:1; 25:2; Yer 9:11; 49:2 Basi Yoshua akauteketeza mji wa Ai, na kuufanya kuwa ni rundo la magofu hata milele, kuwa ni ukiwa hata siku hii ya leo. 29#Yos 10:26,27; Zab 107:40; 110:5; Kum 21:23; Yos 7:26; 10:27; 2 Sam 18:17 Na huyo mfalme wa Ai akamtundika katika mti hadi wakati wa jioni; kisha hapo jua lilipokuchwa Yoshua akaagiza, nao wakauondoa mzoga wake katika huo mti, na kuutupa hapo penye maingilio ya lango la mji, kisha wakaweka pale juu yake rundo kubwa la mawe, hata hivi leo.
Yoshua afanya agano upya
30 #
Kum 27:2-8; Mwa 8:20; 12:7,8; Kut 20:24 Ndipo Yoshua alijenga madhabahu kwa BWANA, Mungu wa Israeli katika mlima Ebali. 31#Kut 20:25; Kum 27:5,6; Kut 20:24 Kama Musa, mtumishi wa BWANA, alivyowaamuru wana wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Torati ya Musa, madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo mtu hakutumia juu yake chombo cha chuma; nao wakatoa juu yake sadaka za kuteketezwa kwa BWANA, na kuchinja sadaka za amani. 32#Kum 27:2,8 Akaandika huko juu ya mawe hayo nakala ya Torati ya Musa, aliyoiandika mbele ya wana wa Israeli. 33#Kum 11:29; 27:11-14; 31:9,12,25; 1 Nya 15:11-13; Law 24:22; Hes 15:16 Na Israeli wote pamoja na wazee, viongozi wao na waamuzi wao, wakasimama upande huu wa sanduku na upande huu, mbele ya makuhani Walawi, waliolichukua sanduku la Agano la BWANA, huyo aliyekuwa mgeni pamoja na huyo mzalia; nusu yao mbele ya mlima Gerizimu, na nusu yao mbele ya mlima Ebali, kama Musa, mtumishi wa BWANA, alivyoamuru hapo awali, ili wawabariki watu wa Israeli. 34#Kum 31:11; Neh 8:3; Kum 29:20,21; 30:19 Na baadaye alisoma maneno yote ya torati, baraka na laana, sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati. 35#Kum 31:12; Kut 12:38; Zek 8:23 Hapakuwa na hata neno moja katika hayo aliyoamuru Musa, ambalo Yoshua hakulisoma mbele ya kusanyiko lote la Waisraeli, na mbele ya wanawake, na watoto, na wageni waliokaa nao.
Iliyochaguliwa sasa
Yoshua 8: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.