Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mambo ya Walawi 11

11
Vyakula halali na haramu
1BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 2#Kum 14:4; Eze 4:4; Dan 1:8; Mt 15:11; Mdo 10:12; Rum 14:2; 1 Kor 8:8; Kol 2:16; Ebr 9:10 Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi. 3Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu iliyopasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala. 4Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 5Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 6#1 Tim 4:4,5 Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 7#Isa 65:4; 66:3,17 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. 8#Isa 52:11; Mt 15:11,20; Mk 7:2,15,18; Mdo 10:14,15; 15:29; Rum 14:14,17; 1 Kor 8:8; Kol 2:16,21; Ebr 9:10 Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.
9 # Kum 14:9,10 Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao. 10#Law 7:18; Kum 14:3 Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu, 11watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu. 12Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu.
13 # Kum 14:12; Rum 14:1-23 Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu; 14na mwewe, na kozi kwa aina zake, 15na kila kunguru kwa aina zake; 16na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; 17na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa; 18#Zab 102:6; Sef 2:14 na mumbi, na mwari, na mderi; 19na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo.
20Tena vyote vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne, hivi ni machukizo kwenu. 21Pamoja na hayo, hivi vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne ni halali kula, hao walio na miguu mirefu, ya kurukia juu ya nchi; 22#Mt 3:4; Mk 1:6; Amu 6:5; Yer 46:23; Nah 3:17 katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake. 23Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu.
Wanyama walio haramu
24Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni; 25#Law 14:8; 15:5; Hes 19:10,22; 31:24 na mtu awaye yote atakayechukua chochote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni. 26Kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, naye hana kwato mbili, wala hacheui, huyo ni najisi kwenu; kila agusaye wanyama hao atakuwa ni najisi. 27Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni. 28Na huyo atakayechukua mzoga wa wanyama hao atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni; hao ni najisi kwenu.
29 # Ebr 9:10; Isa 66:17 Miongoni mwa viumbe watambaao juu ya nchi, hawa ni najisi kwenu; kicheche, panya na mjombakaka kwa aina zake, 30#Zab 58:8; Isa 2:20 na guruguru kenge, mjusi, goromoe na lumbwi. 31Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; yeyote atakayewagusa, wakiisha kuwa mgoza, atakuwa ni najisi hata jioni. 32#Law 15:12 Tena kitu chochote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; cha mti, nguo, ngozi, gunia, chombo chochote cha kufanyia kazi yoyote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hadi jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi. 33#Law 6:28 Na kila chombo cha udongo, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, kila kilichomo ndani yake kitakuwa ni najisi, na hicho chombo kitavunjwa. 34Chakula chochote cha kuliwa kitakuwa najisi kikitiwa maji ya chombo hicho; na kila kinyweo ambacho ni cha kunywewa, kilichomo katika chombo kama hicho, kitakuwa ni najisi. 35Na kila kitu kitakachoangukiwa na kipande chochote cha mizoga yao kitakuwa najisi; iwe ni tanuri, au meko ya vyungu, kitavunjwa vipande vipande; ni najisi vitu hivyo, navyo vitakuwa najisi kwenu. 36Pamoja na hayo, chemchemi, au shimo, ambamo maji yakusanyika, vitakuwa ni safi; lakini hicho kitakachogusa mizoga yao kitakuwa ni najisi. 37Na kipande chochote cha mzoga kikiwa kimeangukia mbegu za kupandwa, zitakazopandwa zitakuwa safi. 38Lakini ikiwa hizo mbegu zilitiwa maji na chochote cha mizoga yao kuziangukia, ni najisi kwenu.
39Mnyama yeyote ambaye mna ruhusa kumla akifa, yeye anayeugusa mzoga wake atakuwa najisi hadi jioni. 40#Law 17:5; 22:8; Kum 14:21; Eze 4:14; 44:31 Na yeye atakayekula nyama ya mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; yeye atakayeuchukua mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hadi jioni.
41Na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi ni machukizo; hakitaliwa. 42Kila aendaye kwa tumbo lake, na kila aendaye kwa miguu minne, na kila aendaye kwa miguu mingi, maana, ni vyote vyenye kutambaa vitambaavyo juu ya nchi, hamtavila, kwa kuwa ni machukizo. 43#Law 20:25 Msifanye nafsi zenu kuwa ni chukizo kwa kitu chochote chenye kutambaa, kitambaacho, wala msifanye nafsi zenu kuwa ni najisi kwa vitu hivyo, mkajipatia uchafu kwa hivyo. 44#Law 19:2; 1 Pet 1:15,16; Isa 51:15; 43:3; Kut 19:6; 1 The 4:7 Kwa kuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yoyote, kiendacho juu ya nchi. 45#Mwa 35:1,2; Kut 6:7; 20:2; Rum 14:17; 12:1; 1 Kor 6:11 Kwa kuwa mimi ni BWANA niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu.
46Hii ndiyo sheria katika hao wanyama, na ndege, na kila kiumbe kilicho hai, kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi; 47#Law 10:10; Yer 15:19; Eze 22:26; 44:23 ili kupambanua kati ya hao walio najisi na hao walio safi, na kati ya kiumbe kilicho hai ambacho chaliwa, na hicho kilicho hai ambacho hakiliwi.

Iliyochaguliwa sasa

Mambo ya Walawi 11: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia