Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 20:1-8

Luka 20:1-8 SRUV

Ikawa siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri Habari Njema, wakuu wa makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafla; wakamwambia, wakisema, Tuambie, unatenda mambo hayo kwa mamlaka gani? Tena, ni nani aliyekupa mamlaka haya? Akajibu akawaambia, Nami nitawauliza ninyi neno moja; niambieni, Ubatizo wa Yohana, je! Ulitoka mbinguni au kwa wanadamu? Wakaulizana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema ulitoka mbinguni, atasema, Basi, mbona hamkumwamini? Na tukisema ulitoka kwa wanadamu, watu wote watatupiga kwa mawe, kwa kuwa wamemkubali Yohana kuwa ni nabii. Wakajibu, kwamba, Hatujui ulikotoka. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.

Soma Luka 20