Luka 20:1-8
Luka 20:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na waalimu wa sheria pamoja na wazee walifika, wakasema, “Tuambie! Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?” Yesu akawaambia, “Na mimi nitawaulizeni swali: Mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka kwa Mungu au kwa watu?” Lakini wao wakajadiliana hivi: “Tukisema yalitoka kwa Mungu, yeye atatuuliza: ‘Mbona hamkumsadiki?’ Na tukisema yalitoka kwa binadamu, watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohane alikuwa nabii.” Basi, wakamwambia, “Hatujui mamlaka hayo yalitoka wapi.” Yesu akawaambia, “Hata mimi sitawaambia ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.”
Luka 20:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri habari njema, wakuu wa makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafula; wakamwambia, wakisema, Tuambie, unatenda mambo hayo kwa mamlaka gani? Tena, ni nani aliyekupa mamlaka hii? Akajibu akawaambia, Nami nitawauliza ninyi neno moja; niambieni, Ubatizo wa Yohana, je! Ulitoka mbinguni au kwa wanadamu? Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema ulitoka mbinguni, atasema, Basi, mbona hamkumwamini? Na tukisema ulitoka kwa wanadamu, watu wote watatupiga kwa mawe, kwa kuwa wamemkubali Yohana kuwa ni nabii. Wakajibu, kwamba, Hatujui ulikotoka. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.
Luka 20:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri Habari Njema, wakuu wa makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafla; wakamwambia, wakisema, Tuambie, unatenda mambo hayo kwa mamlaka gani? Tena, ni nani aliyekupa mamlaka haya? Akajibu akawaambia, Nami nitawauliza ninyi neno moja; niambieni, Ubatizo wa Yohana, je! Ulitoka mbinguni au kwa wanadamu? Wakaulizana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema ulitoka mbinguni, atasema, Basi, mbona hamkumwamini? Na tukisema ulitoka kwa wanadamu, watu wote watatupiga kwa mawe, kwa kuwa wamemkubali Yohana kuwa ni nabii. Wakajibu, kwamba, Hatujui ulikotoka. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.
Luka 20:1-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Siku moja, Yesu alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, pamoja na wazee wa watu wakamjia. Wakamuuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?” Akawajibu, “Nami nitawauliza swali. Je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?” Wakahojiana wao kwa wao wakisema, “Kama tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ watu wote watatupiga mawe, kwa sababu wanaamini kwamba Yohana alikuwa nabii.” Basi wakajibu, “Hatujui ulikotoka.” Yesu akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”