Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 3

3
Tangazo la Yohana
1Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa mtawala wa Yudea, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene, 2wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, neno la Mungu lilimfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani. 3#Mt 3:1-12; Mk 1:1-8 Akafika katika nchi yote iliyo karibu na Yordani, akihubiri ubatizo wa toba iletayo ondoleo la dhambi, 4#Isa 40:3-5 kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya nabii Isaya;
Sauti ya mtu aliaye nyikani,
Itengenezeni njia ya Bwana,
Yanyosheni mapito yake.
5Kila bonde litajazwa,
Na kila mlima na kilima kitashushwa;
Palipopindika patakuwa pamenyoka,
Na palipoparuza patalainishwa;
6 # Mdo 28:28 Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu.
7 # Mt 12:34; 23:33; Yn 3:36 Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazawa wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? 8#Yn 8:33 Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Abrahamu watoto. 9#Mt 7:19 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa kwenye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. 10Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi? 11Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo. 12#Lk 7:29 Watoza ushuru nao wakaja kubatizwa, wakamwuliza, Mwalimu, tufanye nini sisi? 13Akawaambia, Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa. 14Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtosheke na mishahara yenu.
15 # Yn 1:19-28 Basi, watu walipokuwa wakingoja yatakayotokea, wote wakiwaza mioyoni mwao kuhusu Yohana, kama labda yeye ndiye Kristo, 16#Mdo 13:25 Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza kamba ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto; 17ambaye ungo wake uko mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanja wake wa kupuria, na kuikusanya ngano ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
18Basi, kwa maonyo mengine mengi aliwahubiria watu. 19#Mt 14:3-4; Mk 6:17-18 Lakini mfalme Herode alipokaripiwa na yeye kwa ajili ya Herodia, mke wa nduguye, na maovu yote aliyoyafanya Herode, 20aliongeza na hili juu ya yote, alimfunga Yohana gerezani.
Kubatizwa kwa Yesu
21 # Mt 3:13-17; Mk 1:9-11; Yn 1:32 Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; 22#Mwa 22:2; Zab 2:7; Isa 42:1; Mt 3:17; Mk 1:11; Lk 9:35 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.
Ukoo wa Yesu
23 # Mt 1:1-17 Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri wa miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,#Lk 4:22 24wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, wa Yusufu, 25wa Matathia, wa Amosi, wa Nahumu, wa Esli, wa Nagai, 26wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yusufu, wa Yuda, 27#1 Nya 3:17; Ezr 3:2 wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri, 28wa Melki, wa Adi, wa Kosamu, wa Elmadamu, wa Eri, 29wa Yoshua, wa Eliezeri, wa Yorimu, wa Mathati, wa Lawi, 30wa Simeoni, wa Yuda, wa Yusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu, 31#1 Sam 16:1,13; 2 Sam 5:14 wa Melea, wa Mena, wa Matatha, wa Nathani, wa Daudi, 32#Rut 4:22 wa Yese, wa Obedi, wa Boazi, wa Salmoni, wa Nashoni, 33#1 Nya 2:1-5; Mwa 29:35 wa Aminadabu, wa Admini, wa Hesroni, wa Peresi, wa Yuda, 34#Mwa 21:2,3; 11:10-26; 1 Nya 1:24-27 wa Yakobo, wa Isaka, wa Abrahamu, wa Tera, wa Nahori, 35wa Serugi, wa Regau, wa Pelegi, wa Eberi, wa Sala, 36#Mwa 5:3-32; 1 Nya 1:1-4; Mwa 4:25; 11:10 wa Kenani, wa Arfaksadi, wa Shemu, wa Nuhu, wa Lameki, 37wa Methusela, wa Henoko, wa Yaredi, wa Mahalaleli, wa Kenani, 38#Mwa 5:1-3 wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu.

Iliyochaguliwa sasa

Luka 3: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia