Mathayo 11
11
Wajumbe kutoka kwa Yohana Mbatizaji
1 #
Mt 7:28; 13:53; 19:1; 26:1 Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.
2 #
Lk 7:18-35
Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,#Mt 14:3 3#Mal 3:1; Dan 9:26 Wewe ndiwe yule ajaye, au tumngojee mwingine? 4Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona; 5#Isa 35:5-6; 61:1 vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema. 6#Mt 13:57; 26:31 Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami.
Yesu amsifu Yohana Mbatizaji
7 #
Mt 3:1,5 Na hao walipokwenda zao, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? 8Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme. 9#Lk 1:76 Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na aliye mkuu zaidi ya nabii. 10#Mal 3:1; Mk 1:2; Yn 3:28 Huyo ndiye aliyeandikiwa haya,
Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu
Mbele ya uso wako,
Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.
11 #
Mt 13:17
Lakini, nawaambieni, Hajatokea mtu katika wazawa wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. 12#Lk 16:16; 13:24; Yn 6:15 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu huuteka. 13Kwa maana manabii wote na Torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. 14#Mal 4:5; Mt 17:10-13; Mk 9:11-13 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja. 15Mwenye masikio, na asikie.
16Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wanaokaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakisema, 17#Mit 29:9 Tuliwapigia filimbi, wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia. 18#Mt 3:4 Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Ana pepo. 19#Mt 9:14,15 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
Ole Miji isiyotubu
20 #
Lk 10:12-15
Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu. 21#Isa 23:1-18; Eze 26:1—28:26; Yoe 3:4-8; Amo 1:9-10; Zek 9:2-4; Yon 3:6 Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu. 22Lakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. 23#Isa 14:13-15; Mwa 19:24-28; Mt 4:13; 8:5; 9:1 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo. 24#Mt 10:15; Lk 10:12 Lakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.
Yesu amshukuru Baba yake
25 #
Lk 10:21,22 Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.#1 Kor 1:26-29 26Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. 27#Yn 3:35; 1:18; 10:15; Mt 28:18; Flp 2:9 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia. 28#Mt 12:20; Yer 31:25 Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29#Yer 6:16 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30#1 Yoh 5:3 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Iliyochaguliwa sasa
Mathayo 11: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.