Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko 16:1-8

Marko 16:1-8 SRUV

Na sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. Na alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza; wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi? Hata walipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuvingirishwa; nalo lilikuwa kubwa mno. Wakaingia kaburini wakaona kijana akiwa ameketi upande wa kulia, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu. Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulubiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka. Lakini nendeni zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya; huko mtamwona, kama alivyowaambia. Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; kwa maana wameingiwa na hofu na mshangao; wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa.

Soma Marko 16

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Marko 16:1-8