Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nehemia 5

5
Nehemia akabiliana na udhalimu
1 # Isa 5:7; Yak 5:4; Law 25:35; Kum 15:7 Ndipo kukatokea kilio kikuu cha watu, na wake zao, juu ya ndugu zao Wayahudi. 2#Mwa 41:57; Hag 1:6 Maana, walikuwako watu waliosema, Sisi, na wana wetu na binti zetu, tu wengi; na tupate ngano, tule, tukaishi. 3Tena walikuwako wengine waliosema, Tumeweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu, na nyumba zetu; tupate ngano, kwa sababu ya njaa. 4Tena walikuwako wengine waliosema, Tumekopa fedha ili kulipa kodi ya mfalme kwa kuweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu. 5#Mwa 37:27; Isa 58:7; Mdo 17:26; Kut 21:7; Mt 18:25 Walakini miili yetu ni kama miili ya ndugu zetu, na watoto wetu kama watoto wao; kumbe! Mnawatia utumwani wana wetu na binti zetu kuwa watumishi, na baadhi ya binti zetu wamekwisha kutiwa utumwani; wala hatuwezi kujiepusha na hayo; maana watu wengine wana mashamba yetu na mizabibu yetu. 6#Kut 11:8; Neh 13:8; Mk 3:5; Efe 4:26 Nami nilikasirika sana, niliposikia kilio chao, na maneno hayo. 7#Law 19:17; 1 Tim 5:20; Kut 22:25; Kum 23:19; Zab 15:5; Mit 27:5; Mt 18:17 Ndipo nikafanya shauri na nafsi yangu, nikagombana na wakuu na maofisa, nikawaambia, Nyote mnatoza watu riba, mtu na ndugu yake. Nikakutanisha mkutano mkubwa ili kukabiliana nao. 8#Law 25:48 Nikawaambia, Sisi kwa kadiri ya uwezo wetu tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi, waliouzwa kwa makafiri; na ninyi mnataka kuwauza ndugu zenu, tena kuwauza ili sisi tuwanunue? Wakanyamaza kimya, wasiweze kusema neno lolote. 9#Mwa 20:11; Law 25:36; Mdo 9:31; Mwa 13:7,8; 2 Sam 12:14; Rum 2:24; Tit 2:5; 1 Pet 2:12 Tena nilisema, Neno hili mnalolitenda si jema; je! Haiwapasi ninyi kwenda katika kicho cha Mungu wetu, kwa sababu ya mashutumu ya makafiri adui zetu? 10Isitoshe mimi, ndugu zangu na watumishi wangu, tunawakopesha fedha na ngano ili kujipatia faida? Tafadhali na tuliache jambo hili la riba. 11Naomba, warudishieni hivi leo mashamba yao, mashamba yao ya mizabibu, mashamba yao ya mizeituni, nyumba zao, lile fungu la mia la fedha, la ngano, la divai, na la mafuta, mnalowatoza. 12#Ezr 10:5; Yer 34:8,9 Ndipo wakasema, Tutawarudishia, wala hatutataka kitu kwao; tutafanya hivyo, kama ulivyosema. Kisha nikawaita makuhani, nikawaapisha, ya kwamba watafanya kama walivyoahidi. 13#Mt 10:14; Mdo 13:51; Zek 5:4; 2 Fal 23:3 Tena nikakung'uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung'ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung'utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA. Nao watu wakafanya kama walivyoahidi.
Ukarimu wa Nehemia
14 # Neh 13:6; 1 Kor 9:4 Tena tangu wakati huo nilipowekwa kuwa mtawala wao katika nchi ya Yuda, tangu mwaka wa ishirini hadi mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta mfalme, yaani, miaka kumi na miwili, mimi na ndugu zangu hatukula chakula cha mtawala. 15#2 Kor 11:9; Mwa 42:18; Ayu 31:23; Zab 112:1; Mit 16:6; Mhu 12:13,14; Lk 18:2-4 Lakini watawala wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arubaini za fedha; tena hata watumishi wao nao wakawatawala watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nilimcha Mungu. 16Naam, hata kazi ya ukuta huu tena nikaishika sana, wala hatukujipatia mashamba; na watumishi wangu wote wakakusanyika huko kazini. 17#2 Sam 9:7 Pamoja na hayo wakawako mezani pangu, katika Wayahudi na maofisa, watu mia moja na hamsini, zaidi ya wale waliotujia kutoka kwa mataifa yaliotuzunguka. 18#1 Fal 4:22 Basi, maandalizi ya chakula yaliyoandaliwa kila siku yalikuwa ng'ombe mmoja na kondoo sita wazuri; tena nikaandaliwa kuku, na mara moja katika siku kumi akiba ya mvinyo ya namna zote; wala kwa hayo yote sikudai marupurupu ya chakula cha mtawala, kwa kuwa watu walikuwa wamebeba mzito mzito. 19#Neh 13:22 Unikumbuke, Ee Mungu wangu, kwa mema, wote niliowatendea watu hawa.

Iliyochaguliwa sasa

Nehemia 5: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia