Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 17

17
Kuchipuka kwa fimbo ya Haruni
1Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia, 2Nena na wana wa Israeli, kisha upokee kwao fimbo, fimbo moja kwa ajili ya nyumba ya kila baba, katika wakuu wao wote, kama nyumba za baba zao zilivyo, fimbo kumi na mbili; kisha andika jina la kila mtu katika fimbo yake. 3Na katika fimbo ya Lawi utaliandika jina la Haruni; maana, itakuwa fimbo moja kwa kila kichwa cha nyumba za baba zao. 4#Kut 25:22; 29:42; 30:36; 40:34; Law 16:2; 1 Fal 8:10-12 Nawe utaziweka katika hema ya kukutania mbele ya huo ushahidi, hapo nikutanapo pamoja nanyi. 5#Hes 16:5 Kisha itakuwa, mtu huyo nitakayemchagua, fimbo yake itachipuka nami nitayakomesha manung'uniko ya wana wa Israeli, wanung'unikiayo kwangu juu yenu. 6Basi Musa akawaambia wana wa Israeli, ndipo wakuu wao wote wakampa fimbo, fimbo moja kwa kila mkuu, kama nyumba za baba zao zilivyokuwa, fimbo kumi na mbili; na fimbo ya Haruni ilikuwa kati ya fimbo zao. 7#Kut 38:21; Hes 18:2; Mdo 7:44 Kisha Musa akaziweka hizo fimbo mbele za BWANA katika hema ya kukutania. 8#Ebr 9:4; Mwa 40:10; Zab 110:2; Wim 2:3; Isa 4:2; 9:7; Eze 17:24 Ilikuwa siku ya pili yake, Musa akaingia ndani ya hema ya ushahidi; na tazama, ile fimbo ya Haruni iliyokuwa kwa nyumba ya Lawi ilikuwa imechipuka, imetoa michipukizi, na kuchanua maua; na kuzaa matunda mabivu. 9Kisha Musa akazitoa nje hizo fimbo zote kutoka hapo mbele za BWANA na kuziweka mbele ya wana wa Israeli wote; nao wakaangalia, na kila mtu akaitwaa fimbo yake. 10#Kut 16:32; Hes 31:19-26 Kisha BWANA akamwambia Musa, Irudishe fimbo ya Haruni mbele ya ushahidi, ili itunzwe iwe ishara juu ya hawa wana wa maasi; ili uyakomeshe manung'uniko yao waliyoninung'unikia, ili wasife. 11Basi Musa akafanya hivyo; kama BWANA alivyomwagiza, ndivyo alivyofanya.
12Kisha wana wa Israeli wakanena na Musa, na kumwambia, Angalia, sisi tunakufa, tunaangamia, sote tunaangamia. 13#Hes 18:4,7 Kila mtu akaribiaye, aikaribiaye maskani ya BWANA, hufa; je! Tutakufa sote pia?

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu 17: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia