Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 34

34
Mipaka ya nchi
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Mwa 17:8; Kum 1:7; Zab 78:55; 105:11 Waagize wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapoingia nchi ya Kanaani, (hii ndiyo nchi itakayowaangukia kuwa urithi, maana, hiyo nchi ya Kanaani kama mipaka yake ilivyo,) 3#Yos 15:1; Eze 47:13; Mwa 14:3; Yos 3:16 ndipo upande wenu wa kusini utakuwa tangu bara ya Sini kupita kando ya Edomu, na mpaka wenu wa kusini utakuwa tangu mwisho wa Bahari ya Chumvi kuelekea mashariki; 4#Hes 32:8 kisha mpaka wenu utageuka kwenda upande wa kusini wa kukwelea kwake Akrabimu, kisha kupita kwendelea Sini; na kutokea kwake kutakuwa kuelekea upande wa kusini wa Kadesh-barnea; kisha utaendelea mpaka Hasar-adari, na kufikia Azmoni; 5#Mwa 15:18; 1 Fal 8:65; Isa 27:12 kisha mpaka utageuka kutoka Azmoni kwendelea kijito cha Misri, na kutokea kwake kutakuwa hapo baharini. 6Kisha mpaka wenu wa upande wa magharibi mtakuwa na bahari kubwa na mpaka wake; huu ndio mpaka wenu upande wa magharibi. 7Kisha mpaka wenu wa upande wa kaskazini utakuwa ni huu; kutoka bahari kubwa mtajiandikia mlima wa Hori; 8#Hes 13:21; Yos 13:5,6; 2 Sam 8:9; 2 Fal 14:25; 23:33; Isa 10:9; Yer 39:5; Eze 47:15-20 na kutoka mlima wa Hori mtaweka alama hadi Hamathi; na kutokea kwake mpaka hadi hapo Sedada; 9#Eze 47:17 tena mpaka utatokea hadi Zifroni, na kutokea kwake kutakuwa hapo Hasarenani; huo ndio mpaka wenu wa upande wa kaskazini. 10Kisha mtaweka mpaka wenu wa upande wa mashariki kutoka Hasarenani hadi Shefamu mpaka Ribla; 11#2 Fal 23:33; Yer 39:5; Kum 3:17; Yos 11:2; 19:35 kisha mpaka utateremka kutoka Shefamu mpaka Ribla, upande wa mashariki wa Aini; kisha mpaka utateremka na kufikia upande wa bahari ya Kinerethi#34:11 au ‘Ziwa la Galilaya’. upande wa mashariki; 12kisha mpaka utateremkia Yordani, na kutokea kwake kutakuwa hapo katika Bahari ya Chumvi; hii ndiyo nchi yenu kama mipaka yake ilivyo kuizunguka pande zote. 13#Hes 26:52-56; Yos 14:1,2 Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo BWANA ameagiza wapewe watu wa yale makabila tisa, na nusu ya kabila;#Yos 14:1-5 14#Hes 32:33; Yos 14:2,3 kwa kuwa kabila la wana wa Reubeni kwa nyumba za baba zao, na kabila la wana wa Gadi kwa nyumba za baba zao, wamekwisha pata, na hiyo nusu ya kabila la Manase wamekwisha pata urithi wao; 15hayo makabila mawili na nusu ya kabila wamekwisha pata urithi wao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo Yeriko, upande wa mashariki, kuelekea maawio ya jua.
Viongozi wa makabila
16Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 17#Kut 6:23-25 Haya ndiyo majina ya watu watakaowagawanyia nchi iwe urithi wenu; Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni. 18Kisha mtamtwaa mkuu mmoja wa kila kabila, ili waigawanye nchi iwe urithi wenu. 19#Mwa 29:35; 49:8-10; Kum 33:7; Zab 60:7; 108:8; Hes 13:6,30; Kum 1:36 Na majina ya watu hao ni haya; katika kabila la Yuda, ni Kalebu mwana wa Yefune. 20#Mwa 29:33; 49:5; Eze 48:24 Na katika kabila la wana wa Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi. 21#Mwa 35:18; 49:27; Kum 33:12; Zab 68:27; 80:2 Katika kabila la Benyamini, ni Elidadi mwana wa Kisloni. 22Na katika kabila la wana wa Dani, mkuu, Buki mwana wa Yogli. 23#Mwa 48:8-22; 49:22; Kum 33:13; Zab 80:1 Katika wana wa Yusufu; katika kabila la wana wa Manase, mkuu, Hanieli mwana wa Efodi; 24na katika kabila la wana wa Efraimu, mkuu, Kemueli mwana wa Shiftani. 25Na katika kabila la wana wa Zabuloni, mkuu, Elisafani mwana wa Parnaki. 26Na katika kabila la wana wa Isakari, mkuu, Paltieli mwana wa Azani. 27Na katika kabila la wana wa Asheri, mkuu, Ahihudi mwana wa Shelomi. 28Na katika kabila la wana wa Naftali, mkuu, Pedaheli mwana wa Amihudi. 29#Kum 32:8; Mdo 17:26 Hao ndio BWANA aliowaagiza wawagawanyie urithi wana wa Israeli katika nchi ya Kanaani.

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu 34: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia