Mithali 21
21
1Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA;
Kama mifereji ya maji huugeuza popote apendapo.
2 #
1 Sam 16:7; Yer 17:10; Yn 2:24 Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe;
Bali BWANA huipima mioyo.
3 #
Hos 6:6
Kutenda haki na hukumu
Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.
4 #
Mit 24:20
Mwenye kiburi na moyo wa majivuno,
Taa yake ni dhambi.
5Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu;
Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.
6Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongo
Ni moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti.
7Jeuri ya wabaya itawaondolea mbali;
Kwa sababu wamekataa kutenda hukumu.
8Njia yake aliyelemewa na dhambi imepotoka sana;
Bali mtu aliye safi, kazi yake ni sawasawa.
9Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini,
Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
10 #
Yak 4:5
Nafsi ya mtu mbaya hutamani uovu;
Jirani yake hapati fadhili machoni pake.
11Mwenye mzaha aadhibiwapo, mjinga hupata hekima;
Na mwenye hekima afundishwapo, hupokea maarifa.
12 #
1 Kor 10:10; Rum 2:8 Mwenye haki huitafakari nyumba ya mtu mbaya;
Jinsi wabaya waangushwavyo wakaangamia.
13 #
Zab 58:4; Zek 7:11; Mdo 7:57; Mt 7:2 Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini,
Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa.
14Kipawa cha siri hutuliza hasira;
Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali.
15Ni furaha yao wenye haki kutenda hukumu;
Lakini ni uharibifu kwao watendao maovu.
16Mtu aikosaye njia ya busara
Atakaa katika mkutano wao waliokufa.
17Mtu apendaye anasa atakuwa maskini;
Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri.
18 #
Isa 43:3,4 Mtu asiye haki ni fidia ya wenye haki;
Naye afanyaye hila ni badala ya watu wa adili.
19Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika;
Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.
20 #
Zab 112:3; Mit 10:22; Mt 25:3 Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima;
Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.
21 #
1 Kor 15:58
Aandamaye haki na fadhili,
Ataona uhai na haki na heshima.
22Mwenye hekima huupandia mji wao wenye nguvu;
Na kuziangusha nguvu za tumaini lao.
23Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake,
Atajilinda nafsi yake na taabu.
24Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi;
Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
25Matakwa yake mtu mvivu humwua,
Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi.
26Kuna atamaniye kwa choyo mchana kutwa;
Bali mwenye haki hutoa wala hanyimi.
27Sadaka ya wasio haki ni chukizo;
Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya!
28Shahidi wa uongo atapotea;
Bali mtu asikiaye atasema maneno yadumuyo.
29Asiye haki huufanya uso wake kuwa mgumu;
Bali mtu mnyofu huzifikiri njia zake.
30Hapana hekima, wala ufahamu,
Wala shauri, juu ya BWANA.
31Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita;
Lakini BWANA ndiye aletaye wokovu.
Iliyochaguliwa sasa
Mithali 21: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.