Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 23:26-35

Mithali 23:26-35 SRUV

Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu. Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni mtego wa shimo jembamba. Naam, huotea kama mnyang'anyi; Huwaongeza wenye hila katika wanadamu. Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika. Usiutazame mvinyo iwapo ni mwekundu; uitiapo bilauri rangi yake, ushukapo taratibu; Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka. Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti. Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.

Soma Mithali 23

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mithali 23:26-35