Mithali 29
29
1Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo,
Atavunjika ghafla, wala hapati dawa.
2Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi;
Bali mwovu atawalapo, watu huugua.
3 #
1 Fal 1:48; Flp 2:22; Mit 10:1; 15:20 Apendaye hekima humfurahisha babaye;
Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali.
4Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu;
Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.
5Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake,
Hutandika wavu ili kuitega miguu yake.
6Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya;
Bali mwenye haki huimba na kufurahi.
7 #
Ayu 29:16; Zab 31:7; Isa 35:3,4; Lk 22:32; Gal 6:1 Mwenye haki huyaangalia madai ya maskini;
Bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue.
8Watu wenye dharau huwasha mji moto;
Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu.
9Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu;
Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.
10Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu;
Bali wenye haki humtunza nafsi yake.
11Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote;
Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.
12Mwenye kutawala akisikiliza uongo;
Basi watumishi wake wote watakuwa waovu.
13 #
Mt 5:45
Maskini na mdhalimu hukutana pamoja;
BWANA huwatia nuru macho yao wote wawili.
14 #
Zab 72:2
Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu;
Kiti chake cha enzi kitathibitika milele.
15Fimbo na maonyo hutia hekima;
Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.
16 #
Zab 37:36
Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka;
Bali wenye haki watayatazama maanguko yao.
17 #
Mit 13:24
Mrudi mwanao naye atakustarehesha;
Naam, atakufurahisha nafsi yako.
18 #
1 Sam 3:1; Amo 8:11; Yn 13:17; Yak 1:25 Pasipo maono, watu huacha kujizuia;
Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
19Haitoshi mtumwa kuonywa kwa maneno;
Maana ajapoyafahamu hataitika.
20Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno?
Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
21Amwendekezaye mtumwa wake tangu utoto,
Mwisho wake atakuwa ni mwanawe.
22Mtu wa hasira huchochea ugomvi;
Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana.
23 #
Isa 2:11,12; Mt 23:12; Lk 14:11 Kiburi cha mtu kitamshusha;
Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.
24 #
Law 5:1
Mshiriki wa mwizi huichukia nafsi yake mwenyewe;
Asikia maapizo, wala hana neno.
25 #
Mwa 12:12
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego;
Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.
26Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu;
Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA
27Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki;
Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.
Iliyochaguliwa sasa
Mithali 29: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.