Zaburi 106
106
Ungamo la dhambi za Israeli
1 #
1 Nya 16:34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 100:5; 107:1; 118:1; 136:1; Isa 63:7; Yer 33:11; Mt 19:17 Haleluya.
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 #
Zab 40:5
Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya BWANA,
Au kuzihubiri sifa zake zote?
3 #
Yer 22:15,16; Mt 22:37; Zab 15:2; Mdo 24:16; Gal 6:9 Heri washikao hukumu,
Na kutenda haki sikuzote.
4Ee BWANA, unikumbuke mimi,
Kwa kibali ulicho nacho kwa watu wako.
Unijie kwa wokovu wako,
5Ili niuone wema wa wateule wako.
Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako,
Na kujisifu pamoja na watu wako.
6 #
Law 26:40; 1 Fal 8:47; Dan 9:5 Tumetenda dhambi pamoja na baba zetu,
Tumetenda maovu, tumefanya ubaya.
7 #
Kut 14:10-12
Baba zetu katika Misri
Hawakuzingatia matendo yako ya ajabu;
Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako;
Wakaasi penye bahari, Bahari ya Shamu.
8 #
Yos 7:9; Zab 143:11; Yer 14:7,21 Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake,
Ayadhihirishe matendo yake makuu.
9 #
Kut 14:21-31; Nah 1:4; Isa 63:11 Akaikemea Bahari ya Shamu ikakauka,
Akawaongoza vilindini kana kwamba ni nchi kavu.
10Akawaokoa kutoka kwa mkono wa mtu adui, aliyewachukia,
Na kuwakomboa kutoka kwa mkono wa adui zao.
11Maji yakawafunika watesi wao,
Hakusalia hata mmoja wao.
12 #
Kut 15:1-21
Ndipo walipoyaamini maneno yake,
Waliziimba sifa zake.
13Lakini punde wakayasahau matendo yake,
Wakakosa kungojea ushauri wake.
14 #
Hes 11:4-34
Bali walitamani sana nyikani,
Wakamjaribu Mungu jangwani.
15 #
Isa 10:16
Akawapa walichomwomba,
Lakini akawatumia ugonjwa wa kuwakondesha.
16 #
Hes 16:1-35
Wakamhusudu Musa kambini,
Na Haruni, mtakatifu wa BWANA.
17Nchi ikapasuka ikammeza Dathani,
Ikaufunika mkutano wa Abiramu.
18Moto ukawaka katika mkutano wao,
Miali yake ikawateketeza waovu.
19 #
Kut 32:1-14
Walifanya ndama huko Horebu,
Wakaisujudia sanamu ya kusubu.
20 #
Yer 2:11; Rum 1:23 Wakaubadili utukufu wao
Kuwa mfano wa ng'ombe mla majani.
21Wakamsahau Mungu, mwokozi wao,
Aliyetenda makuu katika Misri.
22Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu,
Mambo ya kutisha penye Bahari ya Shamu.
23 #
Kut 32:10; Kum 9:19; Eze 13:5; 20:13 Akasema ya kuwa atawaangamiza
Kama Musa, mteule wake, asingalisimama,
Mbele zake na kusimama palipobomoka,
Ili aigeuze hasira yake asije akawaangamiza.
24 #
Hes 14:1-35
Wakaidharau nchi ile ya kupendeza,
Wala hawakuliamini neno lake.
25Bali wakanung'unika hemani mwao,
Wala hawakuisikiliza sauti ya BWANA.
26Ndipo alipowainulia mkono wake na kuwaapia,
Ya kuwa atawaangamiza jangwani,
27 #
Law 26:33
Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa,
Na kuwatapanya katika nchi mbali.
28 #
Hes 25:1-13; Kum 4:3; Hos 9:10; Ufu 2:14 Wakamwabudu Baal-Peori,
Wakazila dhabihu zilizotolewa kwa wafu.
29Wakamkasirisha kwa matendo yao;
Tauni ikawashambulia.
30Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu;
Tauni ikazuiliwa.
31Akahesabiwa kuwa ana haki
Kizazi baada ya kizazi hata milele.
32 #
Hes 20:2-13; Yak 3:2 Wakamghadhabisha penye maji ya Meriba,
Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,
33Kwa sababu waliiasi roho yake,
Akasema yasiyofaa kwa midomo yake.
34 #
Amu 1:21; 2:1-3; 3:5-6; Kum 7:2 Hawakuwaangamiza watu wa nchi
Kama BWANA alivyowaambia;
35 #
Amu 3:5; Isa 2:6 Bali walijichanganya na mataifa,
Wakajifunza matendo yao.
36 #
Kut 23:33; Kum 7:10; Amu 2:12; 2 Fal 17:8-11; 2 Nya 33:2-7 Wakazitumikia sanamu zao,
Nazo zikawa mtego kwao.
37 #
Kum 12:30,31; Isa 57:5; Eze 16:20; 2 Fal 17:17 Naam, walitoa wana wao na binti zao
Kuwa dhabihu kwa mashetani.
38 #
Hes 35:33
Wakamwaga damu isiyo na hatia,
Damu ya wana wao na binti zao,
Waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani;
Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.
39Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao,
Wakafanya uasherati kwa matendo yao.
40 #
Amu 2:14-18
Hasira ya BWANA ikawaka juu ya watu wake,
Akauchukia urithi wake.
41 #
Amu 2:14; Neh 9:27 Akawatia mikononi mwa mataifa,
Nao waliowachukia wakawatawala.
42Adui zao wakawaonea,
Wakatiishwa chini ya mkono wao.
43Mara nyingi aliwaponya,
Bali walikuwa wakimwasi kwa mashauri yao,
Wakawa dhalili kwa uovu wao.
44 #
Amu 10:10
Lakini aliyaangalia mateso yao,
Aliposikia kilio chao.
45 #
Law 26:41; Omb 3:32 Akawakumbukia agano lake;
Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;
46 #
Ezr 9:9; Yer 42:12 Akawajalia kuhurumiwa
Na watu wote waliowateka.
47 #
1 Nya 16:35-36; Lk 1:74; 2 Kor 5:15 Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe,
Utukusanye kwa kututoa katika mataifa,
Tulishukuru jina lako takatifu,
Tuzifanyie shangwe sifa zako.
48Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli,
Tangu milele hata milele.
Watu wote na waseme, Amina.
Haleluya.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 106: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.