Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 114

114
Maajabu ya Mungu wakati wa kutoka Misri
1 # Kut 12:51 Haleluya.
Israeli alipotoka Misri,
Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
2Yuda ilikuwa patakatifu pake,
Israeli milki yake.
3 # Kut 14:21; Yos 3:16 Bahari iliona ikakimbia,
Yordani ilirudishwa nyuma.
4 # Zab 29:6; 68:16; Hab 3:6 Milima iliruka kama kondoo dume,
Vilima kama wana-kondoo.
5Ee bahari, una nini, ndio ukimbie?
Yordani, ndio urudi nyuma?
6Enyi milima, ndio mruke kama kondoo dume?
Enyi vilima, kama wana-kondoo?
7Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana,
Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.
8 # Kut 17:1-7; Hes 20:2-13; Zab 107:35 Augeuzaye mwamba kuwa ziwa la maji,
Jiwe gumu kuwa chemchemi.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 114: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia