Zaburi 123:1-4
Zaburi 123:1-4 SRUV
Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni. Kama vile macho ya watumishi Yanavyoutegemea mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Yanavyoutegemea mkono wa bimkubwa wake; Ndivyo macho yetu yanavyomtegemea BWANA, Mungu wetu, Hadi atakapoturehemu. Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu sisi, Kwa maana tumeshiba dharau. Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, Na dharau ya wenye kiburi.