Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 124:1-8

Zaburi 124:1-8 SRUV

Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa, Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia. Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu. Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu; Papo hapo maji yafurikayo Yangalipita juu yetu. Na ahimidiwe BWANA; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. Msaada wetu u katika jina la BWANA, Aliyeziumba mbingu na nchi.

Soma Zaburi 124