Zaburi 136
136
Uumbaji wa Mungu na matukio ya kihistoria
1 #
1 Nya 16:34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 100:5; 106:1; 107:1; 118:1; Yer 33:11 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 #
Kut 18:11; Kum 10:17 Mshukuruni Mungu wa miungu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
3 #
1 Tim 6:15; Ufu 17:14 Mshukuruni Bwana wa mabwana;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
4Yeye peke yake afanya maajabu makuu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
5 #
Mwa 1:1; Mit 3:19 Yeye aliyeumba mbingu kwa fahamu zake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
6 #
Mwa 1:2; Yer 10:12 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
7 #
Mwa 1:16; Kum 4:19 Yeye aliyeumba mianga mikubwa;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
8Jua litawale mchana;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
9Mwezi na nyota zitawale usiku;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
10 #
Kut 12:29
Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wao wa kwanza;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
11 #
Kut 12:51
Akawatoa Waisraeli katikati yao;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
12Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
13 #
Zab 78:13; Kut 14:21-29 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
14Akawavusha Israeli katikati yake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
15Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
16 #
Kum 8:15
Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
17Yeye aliyewapiga wafalme wakuu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
18 #
Kum 29:7
Akawaua wafalme mashuhuri;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
19 #
Hes 21:21-30
Sihoni, mfalme wa Waamori;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
20 #
Hes 21:31-35
Na Ogu, mfalme wa Bashani;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
21 #
Yos 12:1
Akaitoa nchi yao iwe urithi;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
22Urithi wa Israeli mtumishi wake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
23 #
Mwa 8:1; Kum 32:36; Zab 102:17; Isa 63:9; Lk 1:48 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
24Akatuokoa na watesi wetu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
25 #
Zab 104:27
Yeye akipaye kila kiumbe chakula chake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
26Mshukuruni Mungu wa mbingu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 136: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: