Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 26

26
Ombi la haki na ungamo la wema
Ya Daudi.
1 # Zab 7:8; 28:7; Mit 29:25 Ee BWANA, unihukumu mimi,
Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu,
Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.
2Ee BWANA, unijaribu na kunipima;
Unisafishe akili yangu na moyo wangu.
3Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu,
Nami nimekwenda katika kweli yako.
4 # Zab 1:1; Yer 15:17 Sikai pamoja na watu waovu,
Wala sitaingia kuwa pamoja na wanafiki.
5 # Zab 5:5; 15:4; 31:6 Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya,
Wala sitaketi pamoja na watu waovu.
6 # Kut 30:19; Zab 73:13; 1 Tim 2:8 Nitanawa mikono yangu bila ya kuwa na hatia,
Na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA
7Ili niitangaze sauti ya kushukuru,
Na kuzisimulia kazi zako za ajabu.
8BWANA, nimependa makao ya nyumba yako,
Na mahali pa maskani ya utukufu wako.
9Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji,
Wala uhai wangu pamoja na wauaji.
10Mikononi mwao mna madhara,
Na mkono wao wa kulia umejaa rushwa.
11Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu;
Unikomboe, unifanyie fadhili.
12Mguu wangu umesimama palipo sawa;
Katika kusanyiko kuu nitamhimidi BWANA.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 26: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia