Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 41

41
Hakikisho la msaada wa Mungu na ombi la uponyaji
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 # Mit 14:21; Mk 10:21 Heri amkumbukaye mnyonge;#41:1 Au maskini.
BWANA atamwokoa siku ya taabu.
2BWANA atamlinda na kumhifadhi hai,
Naye atafanikiwa katika nchi;
Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.
3BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.
Katika ugonjwa wake unamponya maradhi yake yote.
4 # Zab 6:2 Nami nilisema, BWANA, unifadhili,
Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi.
5Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya,
Atakufa lini, jina lake lipotee?
6 # Zab 12:2 Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo,
Moyo wake hujikusanyia maovu,
Naye atokapo nje huyanena.
7Wote wanaonichukia wananong'onezana juu yangu,
Wananiwazia yaliyo mabaya zaidi.
8Wanafikiri pigo liualo limemshika,
Akalala asiweze kusimama tena.
9 # Mt 26:23; Oba 1:7; Mk 14:18; Lk 22:21; Yn 13:18 Hata rafiki yangu mwandani niliyemtumaini,
Aliyekula pamoja nami,
Ameniinulia kisigino chake.
10Lakini Wewe, BWANA, unifadhili,
Uniinue nipate kuwalipa.
11Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami,
Kwa kuwa adui yangu hajivunii kunishinda.
12 # Zab 34:15; Mdo 2:28 Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza,
Umeniweka mbele za uso wako milele.
* * *
13 # Zab 106:48 Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli,
Tangu milele hata milele. Amina na Amina.
KITABU CHA PILI

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 41: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia