Zaburi 54
54
Sala ya uthibitisho
Kwa mwimbishaji: kwa ala za nyuzi za muziki. Utenzi wa Daudi, wakati Wazifu walipoenda na kumwambia Sauli, “Daudi amejificha kwetu”.
1Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe,
Na kwa uweza wako unifanyie hukumu.
2Ee Mungu, uyasikie maombi yangu,
Uyasikilize maneno ya kinywa changu.
3Kwa maana wageni wamenishambulia;
Watu watishao wananitafuta nafsi yangu;
Hawakumweka Mungu mbele yao.
4 #
Zab 118:7; Isa 41:10; Rum 8:31,32; Ebr 13:6 Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia;
Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.
5 #
Zab 89:49
Atawarudishia adui zangu ubaya wao;
Uwaangamize kwa uaminifu wako.
6Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu;
Ee BWANA, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.
7Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu;
Na jicho langu limeridhika
Kwa kuwatazama adui zangu.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 54: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: