Zaburi 56
56
Kumtumaini Mungu katika mateso
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Njiwa Mkimya wa Mbali. Utenzi wa Daudi alipokamatwa na Wafilisti kule Gathi.
1 #
Zab 31:9
Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza,
Mchana kutwa ananionea akileta vita.
2 #
Zab 57:3
Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa,
Maana ni wengi wanaonipiga vita.
3 #
1 Sam 30:6; 2 Nya 20:3 Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;
4 #
Ebr 13:5,6 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.
Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;
Mwenye mwili atanitenda nini?
5Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu,
Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.
6 #
Mdo 4:27,28 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu,
Kwa kuwa waliniotea ili waniue.
7Je! Wataokoka kwa uovu wao?
Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.
8 #
Mal 3:16
Umehesabu kutangatanga kwangu;
Uyatie machozi yangu katika chupa yako;
(Je! Hayamo katika kitabu chako?)
9 #
Isa 8:9,10 Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo.
Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;
10Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.
Kwa msaada wa BWANA nitalisifu neno lake.
11Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;
Mwanadamu atanitenda nini?
12 #
Zab 116:14-16
Ee Mungu, nadhiri zako ziko juu yangu;
Nitakutolea dhabihu za kushukuru.
13 #
Ayu 33:30
Maana umeniponya nafsi yangu na mauti;
Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke?
Ili niende mbele za Mungu
Katika nuru ya walio hai.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 56: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.