Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 58

58
Sala ya kutaka kisasi
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Utenzi wa Daudi.
1Ni kweli, enyi wakuu, mnanena haki?
Enyi wanadamu, mnahukumu kwa adili?
2 # Zab 94:20 Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu;
Mikono yenu wenyewe inaeneza udhalimu katika nchi.
3 # Zab 51:5 Waovu hupotoka hata kabla ya kuzaliwa kwao;
Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
4 # Zab 140:4 Wana sumu mfano wa sumu ya nyoka;
Wao ni kama fira kiziwi azibaye sikio lake.
5Asiyeisikiliza sauti ya waganga,
Ijapo wanafanya uganga kwa ustadi.
6 # Ayu 4:10 Ee Mungu, uyavunje meno yao vinywani mwao;
Ee BWANA, uyavunje magego ya wanasimba.
7Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi;
Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu.
8Kama konokono ayeyukaye na kutoweka,
Kama mimba iliyoharibika, isiyoliona jua,
9 # Mit 10:25 Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba,
Ataipeperusha kama chamchela,
Iliyo mibichi na iliyo moto.
10 # Kum 32:42; Ayu 22:19; Zab 18:47; Mit 10:11; Ufu 18:20 Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi;
Ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki.
11 # Rum 2:6-11; Ayu 34:11; Mhu 5:8; Yer 32:19; Eze 7:27; Rum 14:12; Ufu 2:23 Na mwanadamu atasema,
Hakika iko thawabu yake mwenye haki.
Hakika yuko Mungu
Anayehukumu katika dunia.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 58: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia