Zaburi 61
61
Hakikisho la ulinzi wa Mungu
Kwa mwimbishaji: kwa ala za nyuzi za muziki. Ya Daudi.
1Ee Mungu, ukisikie kilio changu,
Uyasikilize maombi yangu.
2 #
1 Tim 2:8
Toka mwisho wa nchi nitakulilia ninapozimia moyo,
Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.
3 #
Mit 18:10
Kwa maana ulikuwa kimbilio langu,
Ngome yenye nguvu adui asinipate.
4 #
Zab 15:1; 23:6; Ufu 3:12 Nitakaa katika hema yako milele,
Na kupata kimbilio chini ya mbawa zako.
5 #
1 Kor 3:21-23
Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu.
Umewapa urithi wao waliogopao jina lako.
6Utaziongeza siku za mfalme,
Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.
7 #
Zab 41:12; Lk 1:32 Atakaa mbele za Mungu milele,
Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi.
8 #
Zab 56:12
Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima,
Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 61: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.