Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 63

63
Faraja na uhakikisho katika Bwana
Zaburi ya Daudi, alipokuwa katika Jangwa la Yudea.
1 # 1 Sam 23:14 Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu,
Mwili wangu wakuonea shauku,
Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
2 # 1 Nya 16:11 Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,
Nizione nguvu zako na utukufu wako.
3 # Yn 3:16 Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai;
Midomo yangu itakusifu.
4Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;
Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
5 # Zab 17:15; Isa 25:6 Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono;
Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
6 # Zab 149:5 Ninapokukumbuka kitandani mwangu,
Ninakutafakari usiku kucha.
7 # 2 Kor 1:10 Maana Wewe umekuwa msaada wangu,
Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
8 # Isa 26:9 Nafsi yangu inaambatana nawe sana;
Mkono wako wa kulia unanitegemeza.
9Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiangamiza,
Wataingia katika vilindi vya nchi.
10Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga,
Watakuwa riziki za mbwamwitu.
11 # Sef 1:5 Bali mfalme atamfurahia Mungu,
Kila aapaye kwa Yeye atashangilia,
Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 63: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia