Zaburi 87
87
Shangwe ya kuishi Sayuni
Ya Wakorahi. Zaburi. Wimbo.
1Msingi wake upo
Juu ya milima mitakatifu.
2BWANA ayapenda malango ya Sayuni
Kuliko maskani zote za Yakobo.
3 #
Isa 60:1
Mambo makuu yanasemwa kukuhusu,
Ee Mji wa Mungu.
4Nitataja Rahabu na Babeli
Miongoni mwao wanaonijua.
Tazama Filistia, na Tiro, na Kushi;
Wanasema, Huyu alizaliwa humo.
5 #
Eze 48:35; Mt 16:18 Naam, kuhusu Sayuni yatasemwa,
Huyu na huyu alizaliwa humo.
Na Yeye Aliye Juu
Atauimarisha.
6 #
Zab 22:30; Isa 4:3; Yer 3:19; Eze 13:9 BWANA ataweka kumbukumbu, awaandikapo mataifa,
Huyu alizaliwa humo.
7Waimbao na wachezao ngoma na waseme,
Visima vyangu vyote vimo mwako.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 87: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.