Zaburi 9
9
Uwezo wa Mungu na haki yake
Kwa mwimbishaji: kwa kufuata mtindo wa Muth-labeni. Zaburi ya Daudi.
1Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote;
Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu;
2Nitafurahi na kukushangilia;
Nitaliimbia sifa jina lako, Wewe Uliye juu.
3Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma;
Hujikwaa na kuangamia mbele zako.
4Kwa maana umenifanyia hukumu na haki
Umeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki.
5 #
Kum 9:14
Umewakemea mataifa;
Na kumwangamiza mdhalimu;
Umelifuta jina lao milele na milele;
6Adui wameangamia na kuwa magofu milele.
Nayo miji yao uliing'oa;
Hata kumbukumbu lao limepotea.
7 #
Zab 90:2; Mik 5:2; Hab 1:12; Ebr 1:11 Bali BWANA atakaa milele,
Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu.
8Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki;
Atawaamua watu kwa uadilifu.
9BWANA atakuwa ngome kwake aliyeonewa,
Naam, ngome kwa nyakati za shida.
10 #
Zab 91:14; Yn 17:3; 2 Kor 4:6; 2 Tim 1:12; 1 Yoh 2:3,4 Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe,
Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.
11Mwimbieni BWANA akaaye Sayuni,
Yatangazeni kwa watu matendo yake.
12Maana mlipiza kisasi cha damu awakumbuka,
Hakukisahau kilio cha wanyonge.
13Wewe, BWANA, unifadhili,
Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia;
Wewe uniinuaye katika malango ya mauti,
14 #
Zab 13:5
Ili nizisimulie sifa zako zote;
Katika malango ya binti Sayuni
Nitaufurahia wokovu wako.
15Mataifa wamezama katika shimo walilolichimba;
Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao.
16 #
Kut 7:5
BWANA amejidhihirisha na kutekeleza hukumu;
Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake.
17 #
Ayu 8:13; Zab 50:22; Yer 2:32; Hos 2:13 Wadhalimu wataenda kuzimu,
Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
18 #
Zab 12:5; Flp 1:20 Kwa maana mhitaji hatasahauliwa daima;
Matumaini ya wanyonge hayatapotea milele.
19Inuka, ee BWANA, mwanadamu asipate nguvu,
Mataifa wahukumiwe mbele zako.
20Uwatie hofu, ee BWANA,
Watu wa mataifa na wajitambue kuwa wao ni binadamu tu!
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 9: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.