Ufunuo 11
11
Mashahidi wawili
1 #
Eze 40:3; Zek 2:1-2; 2 Kor 6:16 Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wanaosujudu humo. 2#Lk 21:24; Isa 63:18; Lk 21:24; Zab 79:1; Dan 8:10; Ufu 12:6,14; 13:5 Na behewa lililo nje ya hekalu uliache nje wala usilipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili. 3Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, wakiwa wamevikwa magunia. 4#Zek 4:3,11-14 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi. 5#2 Fal 1:10; 2 Sam 22:9; Yer 5:14 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. 6#1 Fal 17:1; Kut 7:17-19,20; 1 Sam 4:8 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo. 7#Dan 7:3,7,21; Ufu 13:1,5-7; 17:8 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua. 8#Isa 1:9-10; Lk 13:34 Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulubiwa. 9Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini. 10#Zab 105:38 Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi. 11#Eze 37:5,10; Mwa 15:12 Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama kwa miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama. 12#2 Fal 2:11 Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama. 13#Ufu 6:12; 16:18; Eze 38:19,20; Dan 2:19 Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliobakia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.
14 #
Ufu 9:12; 12:12 Ole wao, pigo la pili limekwisha pita, tazama pigo la tatu linakuja punde.
Tarumbeta ya saba
15 #
Kut 15:18; Dan 2:44; 7:14,27; Zek 14:9; Oba 1:21; Zab 2:2; 10:16; 22:28 Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele. 16#Ufu 4:4,10; 7:11 Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifudifudi, wakamsujudia Mungu 17#Kut 3:14; Isa 41:4; Ufu 4:8; 18:8 wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki. 18#Zab 2:1,5,12; 46:6; 99:1; 110:5; 115:13; Ufu 15:1; Rum 2:5; Amo 3:7; Zek 1:6; Dan 9:6,10 Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumishi#11:18 katika Kigiriki ni ‘watumwa’. wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi.
19 #
Ufu 4:5; 8:5; 15:5; 16:18,21; 1 Fal 8:1,6; 2 Nya 5:7; Kut 9:24; 19:16 Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua kubwa ya mawe.
Iliyochaguliwa sasa
Ufunuo 11: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.