Ruthu 1
1
Familia ya Elimeleki yaenda Moabu
1 #
Amu 2:16; Mwa 12:10; 26:1; Kum 28:38; 1 Fal 18:2; 2 Fal 8:1; Amu 17:8; Mik 5:2 Hapo zamani Waamuzi walipokuwa wanatawala, njaa ilitokea katika nchi. Mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaondoka akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili. 2#Mwa 35:19; Amu 3:30 Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki,#1:2 Elimeleki: maana yake ni ‘Mungu ni Mfalme’. #1:2 Naomi: maana yake ni ‘Mwema’. #1:2 Maloni: maana yake ni ‘Ugonjwa’. #1:2 Kilioni: maana yake ni ‘Upotevu’. na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili Maloni na Kilioni, Waefrata wa Bethlehemu ya Yuda. Wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko. 3Akafa Elimeleki, mumewe Naomi; na yule mwanamke akasalia na wanawe wawili. 4Nao wakaoa wanawake wa Kimoabu, jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili Ruthu. Baada ya kukakaa huko miaka kumi hivi, 5wote wawili Maloni na Kilioni wakafa; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.
Naomi na wakweze Wamoabi
6 #
Kut 4:31; Zab 80:14; Yer 29:10; Sef 2:7; Zek 10:3; Lk 1:68; 7:16; Mwa 28:20; 48:15; Kut 16:4,6; Zab 104:14,16; Mit 30:8; Isa 55:10; Mt 6:11 Ndipo alipoondoka, yeye na wakweze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana akiwa katika nchi ya Moabu alipata habari kuwa BWANA alikuwa amewajia watu wake na kuwapa chakula. 7Basi akatoka pale alipokuwa akiishi, na wakweze wawili pamoja naye; wakashika njia ili kurudi mpaka nchi ya Yuda. 8#Yos 24:15; 2 Tim 1:16 Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; BWANA na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia. 9#Rut 3:1 BWANA na awajalie kuona raha kila mmoja nyumbani kwa mumewe. Kisha akawabusu; nao wakapaza sauti zao wakalia. 10Wakamwambia, La, sivyo; lakini tutarudi pamoja nawe kwa watu wako. 11#Mwa 38:11; Kum 25:5 Naye Naomi akasema, Enyi wanangu, rudini; kwa nini mfuatane nami? Je! Mimi ninao watoto wa kiume tena tumboni mwangu, hata wawe waume zenu? 12Enyi wanangu, mrejee; nendeni zenu; kwa kuwa mimi ni mzee, siwezi kupata mume tena. Kama ningesema, Natumaini; kama ningepata mume hata usiku huu, na kuzaa watoto wa kiume; 13#Amu 2:15; Ayu 19:21; Zab 32:4; 38:2 je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima? Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa BWANA umetoka juu yangu. 14#Kum 4:4; 10:20; Mit 17:17; 18:24; Yn 6:66-69; Ebr 10:39 Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthu akaambatana naye. 15#Yos 24:15-21; Amu 11:24 Naye akasema, Tazama, dada yako amerudi kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urudi nawe ukamfuate dada yako. 16Naye Ruthu akasema,
Usinisihi nikuache,
Nirudi nisifuatane nawe;
Maana wewe uendako nitakwenda,
Na wewe ukaapo nitakaa.
Watu wako watakuwa watu wangu,
Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu;
17 #
1 Sam 3:17; 25:25; 2 Fal 6:31 Pale utakapofia ndipo nitakufa nami,
Na papo hapo nitazikwa;
BWANA anitende vivyo hivyo na kuzidi,
Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.
18 #
Mdo 21:14
Basi alipomwona kuwa amekata shauri kufuatana naye, aliacha kumshawishi.
19 #
Mt 21:10; Isa 23:7; Omb 2:15 Hivyo hao wakaendelea wote wawili hadi walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote uliwaajabia. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi? 20Akawaambia, Msiniite Naomi,#1:20 Tazama Rut 1:2. niiteni Mara#1:20 Mara: maana yake ni, ‘Uchungu’. kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana. 21#1 Sam 2:7,8; Ayu 1:21 Mimi nilitoka nikiwa nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa? 22#Kut 9:31; 2 Sam 21:9 Basi Naomi akarudi; pamoja na Ruthu Mmoabi, mkwewe; ambao walirudi kutoka nchi ya Moabu; nao wakafika Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri.
Iliyochaguliwa sasa
Ruthu 1: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.