Mwanzo 22
22
Abrahamu anamtoa Isaka sadaka#22:1-19 Historia ya Abrahamu inafikia mahali muhimu na pa kufa na kupona kuhusu ahadi ya Mungu kwake. Wakati ambapo ilionekana kwamba Abrahamu atapata mtoto wa kumrithi, na kweli mtoto Isaka akazaliwa, yaani ahadi ya Mungu imetimia, wakati huo anatakiwa amtoe huyo mtoto kuwa kafara, mtoto yule yule aliyeahidiwa. Hata hivyo Abrahamu katika hali hiyo ngumu mno anajionesha kuwa mwaminifu kwa Mungu na anatii. Hivyo Abrahamu amekuwa mfano wa wenye kumwamini Mungu. Taz Yak 2:21.
1Baada ya muda fulani, Mungu alimjaribu Abrahamu. Mungu alimwita, “Abrahamu!” Naye akaitika, “Naam nasikiliza.” 2Mungu akamwambia, “Mchukue mwanao, Isaka, mwanao wa pekee#22:2 Mwanao wa pekee: Ndivyo katika Kiebrania lakini tafsiri ya Kigiriki ya Septuajinta (LXX) badala ya maneno hayo tuna “Mwanao mpendwa”. A.J. linafuata makala ya Septuajinta na kutumia maneno hayo kuhusu Yesu Kristo (Mat 3:17). Taz Efe 1:6. umpendaye, uende mpaka nchi ya Moria,#22:2 Moria: Eneo hilo halijulikani kwa uhakika. Katika 2Nya 3:1 jina la “mlima wa Moria” linataja mahali ambapo Solomoni alijenga hekalu la Yerusalemu. ukamtoe sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuonesha.” 3Basi, kesho yake, Abrahamu akaamka asubuhi na mapema, akatandika punda wake, akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaka mwanawe. Akatayarisha kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kisha akaanza safari kuelekea mahali alipoambiwa na Mungu. 4Mnamo siku ya tatu, Abrahamu aliinua macho akapaona mahali hapo kwa mbali. 5Akawaambia wale watumishi wake, “Ngojeni hapa na huyu punda. Mimi na mwanangu tutakwenda mpaka kule, tukamwabudu Mungu, kisha tutawarudiani.”
6Basi, Abrahamu akazitwaa zile kuni, akamtwika Isaka mwanawe; yeye mwenyewe akachukua moto na kisu mkononi; wakaondoka pamoja. 7Isaka akamwuliza baba yake, “Baba, moto na kuni tunazo; lakini mwanakondoo wa sadaka ya kuteketezwa yuko wapi?” 8Abrahamu akamjibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atatujalia#22:8 Mungu mwenyewe atatujalia: Katika Kiebrania, maneno “Mungu atajalia” ni jina la Mlima. Na “Moria” linatamkika kama Kiebrania cha “Mungu atajalia”. Kitenzi hicho hicho ‘jalia’ kinatumika pia katika aya ya 14. mwanakondoo wa sadaka ya kuteketezwa.” Basi, wakaendelea na safari yao.
9Walipofika mahali ambapo Mungu alimwagiza, Abrahamu akajenga madhabahu na kupanga kuni juu yake. Kisha akamfunga Isaka mwanawe na kumlaza juu ya kuni juu ya madhabahu. 10Abrahamu akaunyosha mkono wake, akatwaa kisu tayari kumchinja mwanawe.
11Lakini malaika wa Mwenyezi-Mungu#22:11 Malaika wa Mwenyezi-Mungu: Taz Mwa 16:7 maelezo. akamwita kutoka mbinguni, “Abrahamu! Abrahamu!” Naye akaitika, “Naam, nasikiliza!” 12Malaika akamwambia, “Usimdhuru mtoto wala usimfanye lolote! Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwani hukuninyima hata mwanao wa pekee.” 13Ndipo Abrahamu akatazama, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake kichakani. Basi, akaenda, akamchukua huyo kondoo, akamtoa sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.#22:13 Kitendo cha kubadili kafara ya binadamu kwa kafara ya mnyama chaweza pia kueleweka kwamba kafara za binadamu hazikubaliki au ni mwiko. Watu wa makabila mengine jirani na Israeli mara kwa mara walitambika kafara za binadamu hasa wakati wa hali ngumu (rejea 2Fal 3:26-27). Tena tunaambiwa mara kadhaa kwamba hata Waisraeli walitambika kafara za binadamu ingawa walikuwa wamekatazwa na sheria ya Mose kufanya hivyo (Lawi 20:1-5). Taz Isa 57:5 maelezo. 14Kwa hiyo, Abrahamu akapaita mahali hapo, “Mwenyezi-Mungu hujalia.” Kama isemwavyo hata leo, “Katika mlima wa Mwenyezi-Mungu, watu hujaliwa.”
15Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni, 16akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimeapa kwa nafsi yangu kwamba kwa kuwa umefanya hivi, wala hukuninyima mwanao wa pekee, 17hakika nitakubariki, na wazawa wako nitawazidisha kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ufuoni mwa bahari. Wazawa wako wataimiliki miji ya adui zao.#22:15-17 Kutokana na utii wa Abrahamu kwa Mungu, Mungu naye anarudia ile ahadi aliyompa (Mwa 12:2 maelezo; rejea Ebr 6:13-14; 11:12). 18Kutokana na wazawa wako mataifa yote duniani yatabarikiwa#22:18 Mataifa yote duniani yatabarikiwa: Kuhusu ahadi hii taz Mwa 12:2-3 maelezo. kwa sababu wewe umeitii amri yangu.” 19Basi, Abrahamu akawarudia wale watumishi wake, nao kwa pamoja wakaondoka, wakarudi Beer-sheba; Abrahamu akakaa huko Beer-sheba.
Watoto wa Nahori#22:20-24 Orodha hii ya nasaba kwa vile inamwingiza hapa Rebeka, mkewe Isaka, inatayarisha simulizi la sura ya 24. Katika orodha wanatajwa watoto kumi na wawili wa Nahori (rejea Mwa 11:27,29). Orodha nyingine inataja watoto kumi na wawili wa Yakobo (Mwa 35:22-26) na watoto kumi na wawili wa Ishmaeli (Mwa 17:20; 25:12-16).
20Baada ya matukio hayo Abrahamu alipata habari kwamba Milka pia amemzalia Nahori, nduguye, watoto wa kiume: 21Usi mzaliwa wa kwanza, Buzi ndugu yake, Kemueli baba yake Aramu, 22Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli. 23Bethueli alimzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori, ndugu yake Abrahamu, watoto hao wanane. 24Zaidi ya hayo, Reuma, suria wa Nahori, pia alimzalia watoto: Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka.
Iliyochaguliwa sasa
Mwanzo 22: BHNTLK
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993

: