Luka 15
15
Mfano wa kondoo aliyepotea
(Mat 18:12-14)
1Siku moja, watozaushuru na wenye dhambi wengi walikwenda kumsikiliza Yesu.#15:1-32 Mifano hii mitatu ya sura ya 15 ina muundo mmoja wa uandishi na maana moja ambayo Yesu anawakabili nayo Mafarisayo ambao walitaka kumkosoa kwa kuhusika na watu wa sifa mbaya (aya 1-2). Kilele cha yote kinaonekana mwishoni mwa mfano wa tatu (aya 25-32). Mungu anahuruma kwa wote hasa waliotupwa au kudharauliwa. Katika Mat 18:12-14 ambayo inafanana na mfano wa kwanza hapa ina maana nyingine. 2Mafarisayo na waalimu wa sheria wakaanza kunung'unika: “Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi,#15:2 Wenye dhambi: Au: watu wa sifa mbaya. Mafarisayo waliwaita hivyo watu ambao hawakufuata sheria kama wao wenyewe na wote walioshughulikia mambo ambayo wao waliyaona kuwa si mema. Waalimu wa sheria na Mafarisayo hawakuweza kukubali kwamba hao watu ambao Yesu alikula pamoja nao walikuwa sawa na wao wenyewe mbele ya Mungu. na tena anakula nao.” 3Yesu akawajibu kwa mfano: 4“Hivi, mmoja wenu akiwa na kondoo 100, akigundua kwamba mmoja wao amepotea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani, na kwenda kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate.#15:4-7 Picha ya mchungaji na kundi lake ni picha tunayopewa mara kwa mara katika Biblia: Isa 40:11; Eze 34. Mfano wa mchungaji unatumiwa juu ya Mungu, juu ya mtawala, juu ya Kristo mwenyewe na pia juu ya viongozi wa Kanisa. 5Akimpata, atambeba mabegani kwa furaha. 6Anapofika nyumbani, atawaita rafiki zake na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami, kwa sababu nimempata yule kondoo wangu aliyepotea.’#15:6 Maneno kupotea, kupata, kufurahi ambayo yanarudiwa katika kila moja ya hiyo mifano mitatu ya sura hii ya 15 (aya: 6,9,32) hulipa umoja wa kimaandishi hilo simulizi na yanatokana na nadharia hiyo moja tu inayozungumziwa. 7Kadhalika nawaambieni, ndivyo kutakavyokuwa na furaha mbinguni#15:7 Mbinguni: labda hapa ni namna ya kumtaja Mungu mwenyewe. kwa ajili ya kutubu kwa mwenye dhambi mmoja, kuliko kwa ajili ya watu tisini na tisa wanaojiona kuwa wema,#15:7 Wema: Yamkini kwa dhihaka kiasi, Yesu anawataja wale wanaoamini kuwa wema na hawaoni haja ya kumrudia Mungu (ling na aya 2). wasiohitaji kutubu.
Sarafu iliyopotea
8“Au mwaonaje? Tuseme mwanamke fulani ana sarafu kumi#15:8 Sarafu kumi: Neno kwa neno: drakma kumi; kiasi cha fedha ambayo thamani yake ilikuwa karibu mshahara wa kutwa wa kibarua wakati huo au dinari. za fedha, akipoteza moja, atafanya nini? Atawasha taa, ataifagia nyumba na kuitafuta kwa uangalifu mpaka aipate. 9Akiipata, atawaita rafiki na jirani zake na kusema, ‘Furahini pamoja nami, kwa sababu nimeipata ile sarafu yangu iliyopotea.’#15:9 Furahini …nimeipata … iliyopotea …: Taz 15:6 maelezo. 10Kadhalika nawaambieni, ndivyo watakavyofurahi malaika wa Mungu kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja anayetubu.”
Mfano wa mwana mpotevu
11Yesu akaendelea kusema, “Kulikuwa na mtu mmoja mwenye watoto wawili wa kiume. 12Yule mdogo alimwambia baba yake: ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Naye akawagawia mali yake.#15:12 Kadiri ya sheria ya Mose (Kumb 21:17), mtoto wa kwanza wa kiume alipata maradufu ya sehemu ya urithi. Kawaida watoto waligawiwa urithi baada ya kifo cha baba yao, lakini kwa sababu maalumu wangeweza kupatiwa sehemu zao baba yao akiwa bado hai. Linganisha Luka 12:13 maelezo. 13Baada ya siku chache, yule mdogo aliuza urithi wake,#15:13 Aliuza urithi wake: Msemo huu wa Kigiriki waweza kutafsiriwa: “akachukua yote”, lakini kulingana na hali yenyewe ya kibiashara inamaanisha kwamba alibadilisha urithi wake kwa fedha. akasafiri na fedha aliyopata, akaenda nchi ya mbali ambako aliitumia ovyo. 14Alipomaliza kutumia kila kitu, kukatokea njaa kali katika nchi ile, naye akaanza kuhangaika. 15Akaomba kazi kwa mwananchi mmoja wa huko naye akampeleka shambani mwake kulisha nguruwe.#15:15-16 Ni dhahiri kwamba nguruwe walikuwa wanyama najisi wasiofaa kuliwa kadiri ya utamaduni wa kidini wa Wayahudi (Lawi 11:7-8; Kumb 14:8), na kwa hiyo yawezekana kwamba huyo bwana tajiri hakuwa Myahudi. Kulisha na kutunza nguruwe ilikuwa kazi iliyodharauliwa na Wayahudi kupita kazi zote, na kutaka kula chakula chao ni hali mbaya tena zaidi. 16Alitamani kula maganda waliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtu aliyempa kitu. 17Alipoanza kupata akili, akafikiri: ‘Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa? 18Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia. 19Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.’ 20Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.
21“Mwanae akamwambia: ‘Baba, nimemkosea Mungu, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao.’ 22Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: ‘Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!#15:22 Baba yake anamrudishia ishara za hadhi yake ya kuwa mtoto wake wa kiume, yaani, mhuri alama ya mamlaka na viatu: alama ya mtu huru (wakati ule watumwa walikwenda miguu mitupu!). 23Mchinjeni ndama mnono; tule na kusherehekea! 24Kwa sababu huyu mwanangu; alikuwa amekufa, kumbe yu hai; alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.’ Wakaanza kufanya sherehe.
25“Wakati huo kaka yake alikuwa bado shambani. Alipokuwa akirudi na kukaribia nyumbani, akasikia vifijo na ngoma.#15:25-32 Kwa kumalizia mfano huo na mwenendo na fikira za yule kaka mkubwa, Yesu anaweka mkazo juu ya mwenendo na fikira za Mafarisayo na waalimu wa sheria ambao hasa ndio anaowahubiria kwa mifano hiyo (tazama pia maelezo ya 15:1-32). 26Akamwita mmoja wa watumishi, akamwuliza: ‘Kuna nini?’ 27Huyo mtumishi akamwambia: ‘Ndugu yako amerudi nyumbani, na baba yako amemchinjia ndama mnono kwa kuwa amempata akiwa salama salimini.’ 28Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hata akakataa kuingia nyumbani. Baba yake akatoka nje na kumsihi aingie. 29Lakini yeye akamjibu: ‘Kumbuka! Miaka yote nimekutumikia, sijavunja amri yako hata mara moja. Umenipa nini? Hujanipa hata mwanambuzi mmoja nikafanye sherehe pamoja na rafiki zangu! 30Lakini mtoto wako huyu aliyekula mali yako pamoja na makahaba, mara tu alipokuja umemchinjia yule ndama mnono.’ 31Baba yake akamjibu: ‘Mwanangu, wewe uko pamoja nami siku zote, na kila nilicho nacho ni chako. 32Ilitubidi kufanya sherehe na kufurahi, kwa sababu huyu ndugu yako alikuwa amekufa, kumbe yu mzima; alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.’”#15:32 Kufurahi …amepotea … amepatikana: Maneno yaleyale ya aya za 6 na 9 lakini sasa yanamkabili kaka yule mkubwa, nayo yanadokezea wale wakuu na viongozi wa dini ambao walijigamba kuwa wamekuwa waaminifu kwa sheria ya Mungu (ling aya 31). Kaka mkubwa hapendi kaka yake mdogo asamehewe!
Iliyochaguliwa sasa
Luka 15: BHNTLK
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993