Luka 8:47-48
Luka 8:47-48 TKU
Yule mwanamke alipoona ya kwamba hataweza kujificha akajitokeza akitetemeka. Akasujudu mbele ya Yesu. Huku kila mmoja akisikia, akaeleza sababu iliyomfanya amguse, na kwamba alipona wakati ule ule alipomgusa. Yesu alimwambia, “Binti yangu umeponywa kwa sababu uliamini. Nenda kwa amani.”