Kumbukumbu la Sheria UTANGULIZI
UTANGULIZI
Kitabu hiki kinaitwa Kumbukumbu la Sheria (Kumbukumbu la Torati katika tafsiri nyingine) kwa kuwa kinarudia tena sheria na maagizo waliyopewa Waisraeli kule mlimani Sinai. Kitabu chenyewe kina masimulizi matatu ambayo Mose aliwaambia Waisraeli (1:1–4:43; 4:44–28:68 na 28:69–30:20.) Mose anayataja mambo Mungu aliyoyafanya kwa ajili ya watu hao kutokana na upendo wake mkuu: Alifanya agano nao, aliwaongoza muda wote wa miaka arubaini kule jangwani, aliwalinda na kuwakinga na maadui zao, akawapa amri na maagizo yake pamoja na ahadi zake. Mose anazungumza na watu hao kama mhubiri hodari wa neno la Mungu na kuwahimiza watu wawe waaminifu kwa Mungu na kuchagua kuwa na uhusiano mwema naye.
Msomaji atakumbuka baadhi ya maneno kadha wa kadha katika kitabu hiki ambayo ni muhimu sana kwa maisha ya watu wa Mungu. “Basi, sikilizeni enyi Waisraeli! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni Mwenyezi-Mungu mmoja! Mpendeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu kwa moyo wote, kwa roho yote na kwa nguvu zote.” 6:4-5 (taz pia Mat 22:37 kuhusu agizo au amri ya kumpenda Mungu). Maneno haya ni ya msingi katika imani ya Waisraeli na yalitumiwa siku kwa siku katika sala.
Katika sura nne za mwisho, yaani 31-34, kuna maandishi mawili ya kishairi na masimulizi mawili: Tunaambiwa juu ya mwongozo na mawaidha kadha wa kadha ambayo Mose aliwapa watu kabla ya kufa kwake. Mose anamteua Yoshua ashike nafasi yake (sura 31), utenzi au wimbo wa Mose (sura 32), Mose anayabariki makabila 12 ya Israeli (sura 33) na mwisho habari za kifo chake Mose (sura 34).
Iliyochaguliwa sasa
Kumbukumbu la Sheria UTANGULIZI: SCLDC10
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Common Language DC Bible: Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki © Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya, 1995, 2001. Haki zote zimehifadhiwa.