Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 10

10
1PALIKUWA na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitaliano, 2mtu nitawa, mcha Mungu, yeye na nyumba yake yote, nae alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu siku zote. 3Akaona katika njozi wazi wazi, panapo saa tissa ya mchana, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, Kornelio! 4Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Maombi yako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. 5Bassi, peleka watu Yoppa, ukamwite Simon, aitwae Petro: 6Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simon, mtengenezaji wa ngozi; nyumba yake iko pwani; atakuambia yakupasayo kutenda. 7Na yule malaika aliyesema nae akiisha kuondoka, Kornelio akaita watumishi wawili wa nyumba yake, na askari mmoja, mtu mtawa, katika wale waliomkhudumia daima: 8na alipokwisha kuwaeleza mambo yote akawatuma kwenda Yoppa.
9Hatta siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, panapo saa sita ya mchana: 10akaingiwa na njaa nyingi, akataka kula: lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia, akaona mbingu zimefunuka, 11na chombo kikimshukia kama nguo kubwa, kinatelemshwa kwa pembe zake nne hatta inchi. 12Ndani yake aina zote za nyama zenye miguu mine, na nyama za mwituni, nazo zitambaazo, na ndege za anga. 13Sauti ikamjia, Ondoka, Petro, ukachinje ule. 14Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijala kamwe kitu kilicho kichafu au najis. 15Sauti ikamjia marra ya pili, Kilichotakaswa na Mungu, usikiite najis. 16Jambo hili likatendeka marra tatu: kiisha kile chombo kikapokewa tena mbinguni.
17Hatta Petro alipokuwa akiona mashaka ndani ya nafsi yake, maana yake nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiislia kuiulizia nyumba ya Simon, wakasimama mbele ya mlango, 18wakaita, wakauliza kwamba Simon aitwae Petro anakaa humo. 19Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutaka. 20Ondoka ushuke ufuatane nao, usione mashaka, kwa maana ni mimi niliyewaleta. 21Petro akawashukia wale watu waliotumwa kwake na Kornelio, akanena, Mimi ndiye mnaemtaka. Mmekuja kwa sababu gani? 22Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mcha Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno yako. 23Akasema, Ingieni; akawakaribisha.
Hatta siku ya pili, Petro akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yoppa wakafuatana nae. 24Hatta siku ya pili yake wakaingia Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwangojea, amekusanya jamaa zake na rafiki zake. 25Petro alipokuwa akiingia, Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia. 26Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwana Adamu. 27Na katika kusema nae akaingia, akaona watu wengi wamekusanyika. 28Akawaambia, Mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi aongee na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, hikini Mungu amenionya, nisimwite mtu awae yote mchafu wala najis. 29Kwa sababu hiyo naiikuja nilipoitwa nisikatae; hassi nauliza, ni neno gani mliloniitia? 30Kornelio akanena, Leo ni siku ya nne tangu nilijiokuwa nikifunga hatta saa hii: na saa tissa nalikuwa nikisali nyumbani mwangu: kumbe! mtu amesimama mbele yangu, mwenye nguo zingʼaazo, akasema, 31Kornelio, maombi yako yamesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu. 32Bassi, tuma watu kwenda Yoppa, ukamwite Simon aitwae Petro, aje hapa; anakaa katika nyumha ya Simon, mtengenezaji wa ngozi, karibu ya pwani: nae akija atasema nawe. 33Marra nikatuma watu kwako, nawe umefanya vyema kuja. Bassi sasa sisi sote tupo hapa mbele za Mungu, tupate kuyasikiliza maneno yote uliyoamriwa na Mungu.
34Petro akafumhua kiuywa chake, akasema, Hakika nimekwisha kutambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; 35bali katika killa taifa mtu amchae na kutenda haki hukuhaliwa nae. 36Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli, akikhubiri amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote), 37jambo lile mmelijua, lililoenea katika Yahudi yote likianzia Galilaya, haada ya ubatizo alioukhubiri Yohana; 38khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae. 39Nasi tu mashahidi ya mambo yote aliyoyatenda katika inchi ya Wayahudi na katika Yerusalemi; ambae walimwua wakamtundika mtini. 40Huyu Mungu alimfufua siku ya talu, akamjalia kudhilurika, 41si kwa watu wote, bali kwa mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na Mungu, ndio sisi, tuliokula na kunywa pamoja nae baada ya kufufuka kwake. 42Akatuagiza tuwakhubiri watu na kushuhudu ya kuwa huyu udiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa hayi na wafu. 43Huyu manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake killa amwaminiye atapewa ondoleo la dhambi.
44Petro alipokuwa akisema maueno haya Roho Mtakatifu akawashukia wote waliosikia maneno yake. 45Na wale waliotahiriwa walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wameshukiwa kipaji cha Roho Mtakatifu. 46Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, wakimwadhimisha Mungu. 47Ndipo Petro akajibu, Aweza mtu kuwakataza hawa maji, wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi? 48Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.

Iliyochaguliwa sasa

Matendo 10: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia